Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo
tarehe 07 Desemba, 2017 amewasili Mkoani Dodoma ambako pamoja na mambo
mengine atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya miaka 56 ya
Uhuru zitakazofanyika katika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma Jumamosi
tarehe 09 Desemba, 2017.
Katika Ikulu ya Chamwino, Mhe. Rais Magufuli amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Satano Mahenge.
Akiwa
Mkoani Dodoma Mhe. Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) atafungua vikao vya Jumuiya za CCM na pia atakuwa mgeni
rasmi katika shughuli mbalimbali za kiserikali.
Mhe. Rais Magufuli ameongozana na Mkewe Mhe. Mama Janeth Magufuli.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
07 Desemba, 2017
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )