Majaji
nchini Ufaransa wamewalaumu wapiganaji walioongozwa na Rais wa sasa wa
Rwanda, Paul Kagame kwa kuilenga na kuiangusha ndege iliyokuwa imembeba
Rais wa wakati huo wa Taifa hilo, Juvenal Habyarimana 1994.
Hii
ni baada ya upelelezi juu ya suala hilo kukamilika. Upelelezi huo
ulikuwa unafanywa na Majaji hao wa Ufaransa juu ya shambulio la kombora
lililosababisha kifo cha Rais Habyarimana na baadaye kusabisha kuanza
kwa mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka huo huo.
Hata hivyo Rwanda nayo inawalaumu Ufaransa kwa kushiriki kupanga mauaji ya kimbari.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )