Kama
ulifikiri kuwa baby Mama wa Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady na
Hamisa Mobetto bifu lao limetulia au kuisha kabisa utakuwa umekosea.
Zari na Hamisa wamekuwa wakiripotiwa kutoelewana na kurushiana vijembe
katika mtandao tangu Hamisa alipozaa na Diamond wakati akijua fika Zari
na muimbaji huyo wa WCB bado ni wapenzi. Sasa Hamisa na Zari si kwamba
wanaviambiana tu kwenye mitandao, bifu lao limeenda mbali zaidi lakini
katika njia ambayo ni nzuri. Wakati Zari akitarajia kufanya event yake
ya Zari All White Party nchini Uganda nyumbani kwao December 21 mwaka
huu, siku hiyo hiyo Hamisa naye ameandaa event yake. Hata hivyo
utakumbuka si mara ya kwanza kwa Zari kufanya party kama hiyo nchini
Uganda na hata Tanzania ameshafanya hivyo lakini kwa Hamisa ni tofauti
kitu ambacho kinatafsiriwa kama bado wanazidizi kuonyeshana umwamba.