Mamlaka
ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), imesema
mifuko ya PSSSF na NSSF iko katika hatua za mwisho za kujenga mifumo ya
ndani ya ulipaji wa fao la upotevu wa ajira, maarufu Fao la Kujitoa.
Vilevile,
imesema Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), utaanza kupokea
maombi ya fao la upotevu wa ajira kuanzia Novemba Mosi, mwaka huu
(Alhamisi), likiwalenga waliopoteza ajira baada ya sheria kuanza kazi
Agosti Mosi, mwaka huu.
Kwa
mujibu wa sheria mpya ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii, kutakuwa na mifuko
miwili nchini ambayo ni PSSSF inayohudumiwa watumishi wa umma ambayo ni
muunganiko wa mifuko ya PSPF, LAPF, PPF na GEPF.
Pia kuna mfuko wa NSSF ambao unahudumia wafanyakazi wa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi.
Hayo
yalisema jana na Meneja Mawasiliano wa SSRA, Sara Kibonde,
alipozungumza na waandishi wa habari waliotaka kujua kama mifuko hiyo
imeshaanza kutoa fao la upotevu wa ajira ambalo limetajwa katika sheria
mpya ya mfuko wa hifadhi ya jamii.
"Kukosekana
kwa utaratibu wa kinga ya kipato kwa wafanyakazi wanaopotea ajira
kumesababisha wafanyakazi kujitoa uanachama na kuchukua michango yao,
ili kujikimu baada ya kupoteza ajira kiasi cha kupewa jina la fao la
kujitoa na hiyo ilitokana na kukosekana kwa mbadala wake," alisema.
Kwa
mujibu wa Kibonde, ukuaji wa sekta binafsi umechangia kuwa na
mabadiliko katika soko la ajira na kuchangia ongezeko la fursa za ajira
zenye masharti ya muda mfupi ya ajira na kusababisha wafanyakazi kuomba
kujitoa uanachama katika mifuko ya hifadhi ya jamii mara mikataba yao ya
ajira inapokoma.
Alibainisha
kuwa takwimu zinaonyesha wafanyakazi walio kwenye kundi la masharti ya
ajira za kudumu ndiyo lina matukio mengi ya wanachama kujitoa.
"Kuwapo
kwa idadi kubwa ya wafanyakazi wanaojitoa kutoka kwenye kundi la
wafanyakazi wenye mikataba ya ajira ya muda mrefu kunaashiria kwamba
baadhi ya wafanyakazi wamekuwa wakijitoa bila sababu za msingi."
Alisema mwanachama anayechukua michango yake anakuwa amepoteza sifa ya kulipwa mafao ya pensheni atakapotimiza umri wa kustaafu na ndiyo maana sheria mpya imeleta utaratibu mbadala ambao utakuwa kinga ya kipato.
Alisema mwanachama anayechukua michango yake anakuwa amepoteza sifa ya kulipwa mafao ya pensheni atakapotimiza umri wa kustaafu na ndiyo maana sheria mpya imeleta utaratibu mbadala ambao utakuwa kinga ya kipato.
Kwa
mujibu wa kanuni za sheria ya mfuko wa hifadhi ya jamii ya mwaka 2018,
utaratibu wa kujitoa kwenye mifuko hiyo umeainishwa kuwa mafao ya
kujitoa yatakuwa asilimia 33.3 ya mshahara wa mwezi wa mwanachama
husika.
Pia,
muda wa ulipaji mafao ni miezi sita na mwanachama atalipwa kwa kipindi
kisichozidi miezi 18 na mwanachama aliyechangia chini ya miezi 18
atalipwa asilimia 50 ya michango yake.
Kanuni
hizo pia zinabainisha kuwa kama mwanachama atakuwa hajapata ajira baada
ya miezi 18, atamwandikia Mkurugenzi Mkuu wa mfuko kuomba kuhamishia
michango yake kwenye mfuko wa hiari na kuendelea kuchangia.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )