Jebra
Kambole, wakili wa mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe
anayeshikiliwa na polisi kituo kikuu cha polisi jijini Dar es Salaam,
amesema mwanasiasa huyo amenyimwa dhamana.
“Polisi
wamesema hawawezi kumuachia kwa leo wanaendelea kumshikilia kwa ajili
ya mahojiano. Wamesema hawawezi kumpa dhamana,” amesema Kambole .
Zitto
alikamatwa na polisi leo saa 5 asubuhi na kupelekwa kituo cha polisi
Oysterbay ambako alihojiwa kwa takribani saa tatu, kisha kuhamishiwa
kituo kikuu cha polisi.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Liberatus Sabas leo
amewaeleza wanahabari kuwa wanamshikilia Zitto kutokana na matamshi
aliyoyatoa hivi karibuni.
Jana,
Jeshi la Polisi mkoani Kigoma lilimtaka Zitto kuwasilisha vielelezo juu
ya kauli aliyoitoa mbele ya waandishi wa habari Jumapili iliyopita
Oktoba 28, 2018 kuwa ana taarifa za wananchi zaidi ya 100 kuuawa katika
tukio la mapigano ya wananchi wa jamii ya Wanyantuzu na polisi wilaya ya
Uvinza mkoani humo.
Kamanda
wa Polisi mkoani Kigoma, Martin Ottieno amesema tuhuma za mbunge huyo
hazina ukweli wowote na kusisitiza kuwa ni upotoshaji unaofanywa na
wanasiasa.
Katika
ufafanuzi wake leo, Kambole amesema Zitto alipofikishwa Oysterbay
aliandika maelezo, kuhojiwa akidaiwa kutoa maneno ya uchochezi.
“Baada
ya kuhojiwa aliandika maelezo ya awali na aliwaeleza kuwa kama kuna
maelezo mengine atayatoa mahakamani,” amesema Kambole.
“Hakuna
chochote kilichoendelea na sheria inamruhusu kama unaona hulazimiki
kutoa maelezo. Maelezo kuhusu makosa yake hajayatoa na hakulazimishwa
kuyatoa anasubiri kama akipelekwa mahakamani atayatoa huko.”
Ameongeza, “Wamesema dhamana yake wameishikilia na kosa lake ni kutoa maneno ya kichochezi.”
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )