Watu
watano wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mikoa ya
Dodoma na Iringa ikiwa ni muda usiozidi saa 24, baada ya kumalizika
mgomo wa madereva wa mabasi na malori.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David
Misime, jana alithibitisha kutokea kwa ajili hiyo ya Dodoma, saa 3:45
usiku, katika eneo la Nzuguni nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Alisema basi hilo lilikuwa likitokea
Mwanza kwenda Morogoro liligongana na gari ndogo aina ya Toyota Mark II
iliyokuwa likiingia barabara kuu kutokea Nzuguni.
“Chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari
dogo kuingia barabarani bila kuwa makini na kusababusha kushindwa kumpa
kipaumbele aliyekuwa barabara kuu kupita kwanza.
“Lakini pamoja na makosa ya gari ndogo, suala la mwendo kasi wa dereva wa basi umesababisha madhara kuwa makubwa,” alisema.
Aliwataja waliopoteza maisha ambao wote
ni waliokuwa katika gari ndogo kuwa ni Askari wa Jeshi la Wananchi
(JWTZ), Monduli mkoani Arusha, Jackson Lazaro aliyekuwa dereva wa gari
dogo.
Wengine waliofariki katika ajali hiyo
ni Mkazi wa Makole, Helena Chiuyo (36), Mwanafunzi wa kidato cha tatu
katika Shule ya Sekondari ya City ya mjini hapa, Fatuma Mtauga (17) na
Mkazi wa Kisasa Stella Giseon (36).
“Dereva wa gari dogo alikuwa akitokea
kijiji Nzuguni kuingia barabara kuu ya Dodoma kuelekea Morogoro
kugongana basi ambalo lilipoteza mwelekeo na kuingia porini umbali
usiopungua mita 300 na kugonga mti na kisha kusimama,”alisema Kamanda
Misime.
Alisema dereva wa basi ambaye ni Mkazi wa Kirumba Mwanza, Leonard Magesa (51) anashikiliwa na polisi kwa mahojiano.
Naye Ofisa Muuguzi wa zamu katika
Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Cecilia Sanya, alisema alipokea majeruhi
huyo saa 6.20 Fatuma Patrick kutoka eneo la ajali akiwa majeraha sehemu
mbalimbali za mwili ikiwemo kichwani .
“Waliongoza na wauguzi wa zamu kwenda
katika eneo la tukio wakiwa na gari la wagonjwa, walivyofika pale
walikuta watu hao wamefariki dunia,” alisema Cecilia.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )