Msanii wa muziki wa Hip Hop, Nay wa
Mitego amesema muziki wa sasa hivi ukileta ufundi na kujifanya unaweza
sana kuchana na kuandika hautafika popote.
Nay wa Mitego amedai ili kwenda kibiashara msanii unatakiwa kubadilika ili kwenda sambamba na mahitaji ya soko.
“Muziki wa kipindi cha nyuma ulikuwa wa
serious sana, ulikuwa unahitaji uumize sana kichwa ili ufanye kitu
kizuri japo ulikuwa hauna hela, lakini muziki wa sasa hivi ni muziki wa
ujanja ujanja mwingi, ukiwa na akili nyingi, ukiwa mjanja basi unamake
mkwanja. Kwa hiyo naweza nikasema muziki wa sasa hivi una hela sana
kuliko wa zamani lakini ili uzipate unatakiwa kuwa mjanja, unaweza ukawa
unachana sana, unaandika sana lakini ukatoka bila,” alisema Nay.
Aliongeza, “Muziki wa sasa hivi ukidumu
kwa muda mrefu ni miezi mitatu, lakini nyimbo nyingi za zamani
zitaendelea kuwepo kwa sababu wasanii wake walikuwa hawana ujanja
ujanja, wanaandika kweli na wanazingatia kila kitu katika uandishi,”
alisema Nay.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )