Jeshi
la Polisi mkoani Simiyu limemfukuza kazi askari wake kwa kudaiwa
kumtorosha mtuhumiwa wa mauaji katika kituo cha Luguru wilayani Itilima,
mkoani hapa.
Pia,
linawashikila askari saba wanaodaiwa kuwatorosha watuhumiwa wengine
watatu wa mauaji na ujangili wilayani Meatu kwa uchunguzi.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi mkoani
Simiyu, Onesmo Lyanga alisema askari huyo amefukuzwa kazi kwa
kulifedhehesha jeshi na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.
“Februali
2, mwaka huu katika Kituo cha Polisi Lugulu, askari alimtorosha
mtuhumiwa wa kesi ya mauaji Itl/Ir/95/2016, mkazi wa Kijiji cha
Gambasingu wilayani Itilima,” alida Kamanda Lyanga.
Hata
hivyo, alisema polisi wanaendelea kuchunguza tukio la kutoroka kwa
watuhumiwa wa ujangili wilayani Meatu, na linaendelea kuwashikilia
askari wengine saba.
Alisema
tukio hilo lilitokea Januari 19, 2016, usiku katika Kituo cha Polisi
Wilaya ya Meatu mkoani hapa na kusababisha watuhumiwa hao kutoboa ukuta
na kutoka.
Kamanda
huyo aliwataja watuhumiwa waliotoroka kuwa ni mkazi wa kijiji cha
Mwasungula aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya mauaji na wengine wawili ni
wakazi wa kijiji cha Sapa wanaotuhumiwa kukutwa na pembe za tembo.
“Watuhumiwa
waliotoroka katika mahabusu siyo ambao walihusika kutungua helkopita na
kusababisha mauaji ya rubani Rogers Gower, raia wa Uingereza kama
baadhi ya vyombo vya habari vilivyo ripoti, watuhumiwa hao wapo,”alisema Lyanga.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )