CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kitaendelea kuimarisha miundombinu na
mazingira rafiki ya kiutendaji kwa kuwapatia vifaa vya kisasa jumuiya
mbali mbali za taasisi hiyo ili zifanye kazi kwa ufanisi.
Kauli
hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Zanzibar,
Najma Murtaza Giga wakati akikabidhi Vifaa mbali mbali kwa Uongozi wa
Wazazi Mkoa wa Mjini, huko Afisi ya CCM Amani.
Amesema taasisi hiyo inatakiwa kwenda sambamba na mabadilio ya sayansi na teknolojia kwa kutumia nyenzo za
kisasa zitakazowasaidia watendaji wa taasisi hizo kufanya kazi nzuri na kwa haraka.
Aidha
amesema chama hicho kitafanya kila kinachowezekana kuhakikisha
kinawapatia Vitendea Kazi Watendaji wa CCM kadri ya uwezo wa kifedha
unaporuhusu.
Giga
amewasihi viongozi mbali mbali wa chama na jumuiya zingine kuunga mkono
juhudi zinazofanywa na jumuiya ya wazazi katika kutoa malezi bora ya
kitaaluma na kisaikolojia kwa watoto kwa lengo la kutengeneza viongozi
makini na weledi wa baadae.
Nae
Katibu wa CCM mkoa wa mjini, Mohamed Omar Nyawenga amewataka watendaji
wa chama hicho kuwa wabunifu na kutumia weledi kwa kufanya kazi kwa bidi
ili kusaiudia chama kutekeleza ilani ya uchaguzi ya 2015/2020 kwa
ufanisi ili wananchi waendelee kuiunga mkono CCM katika chaguzi zote
zijazo.
Vifaa vilivyotolewa ni Kompyuta 2, mashine za Printer 2 na mashine za photocopy 4 kwa jumuiya ya wazazi mkoa wa mjini kichama.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )