Featured
Loading...

Diamond Platnumz Awashukuru Instagram Baada Ya Kumongezea Muda Wa Kupost Video



MSANII wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Nassib Abdul ‘Diamond’ pamoja na watumiaji wengine wa mtandao wa Instagram wameonekana kufurahia kuongezewa nafasi ya kuweka video katika mtandao huo kutoka sekunde 15 hadi 60.

Diamond na watu wengine walituma baadhi ya video zenye urefu wa muda ulioongezwa kama ishara ya kufurahia ukubwa huo ulioongezwa kwenye mtandao huo wenye watumiaji zaidi ya milioni 400 duniani kote.

“From 15 seconds to 1 minute’ mwee! Asante instagram kwa kutuongezea urefu wa hizi ‘clip’ tujinafasi,” aliandika Diamond kwenye video aliyoituma akiwa na mtoto wake kwenye kifaa cha kubeba mtoto akiwa anavutwa

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top