Mkuu
wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema hataki kuwaona nyumbani
kwake wasanii ambao wamekacha kuhudhuria kampeni yake ya usafi ambayo
imezinduliwa Jumamosi hii katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es
salaam.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Paul Makonda ameonesha kusikitishwa na idadi ndogo ya wasanii waliojitokeza kuunga mkogo kampeni hiyo.
“Lakini
nashukuru wasanii wote ambao wamejumuika nasi, na kwa kweli hiki ni
kipimo cha kuwatambua marafiki zangu wa kweli ni wapi. Na mimi niwaambie
tu, sitaki kuona msanii yoyote nyumbani kwangu ambaye hawezi kuniunga
mkono kwenye mambo yangu ya maendeleo,” alisema Makonda.
“Sitaki
hiyo tabia, nimemuona Steve Nyerere hapa amekuja akiwa amechelewa hilo
ni onyo, ukirudia tena nakushughulikia. Huwezi kuwa rafiki yangu alafu
kwenye mambo kama haya huhangaiki, wengine wanataka waombwe, eti mbona
hujanipigia simu kuniomba nipost, we nani?. Swala la usafi siyo la
serikali ni swala la kila mtu,” aliongeza Makonda.
Wasanii
ambao walihudhuria uzinduzi huo ni, Mchizi Mox, Yamoto Band, Diamond na
team ya Wasafi, Mwasiti, Queen Darleen, Salam TMK pamoja na Steve
Nyerere wa bongo movies.
Katika hatua nyingine Makonda amevitaka vyombo vya usafiri jijini Dar es salaam kuwa na vifaa vya kuwekea uchafu.
Pia
wamewataka wafanyabiashara siku ya jumamosi, kufungua maduka yao saa 3
asubuhi ili muda wa asubuhi wautumie kwa ajili ya kufanya usafi.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )