Featured
Loading...

Said Fella aisupport kiaina diss ya Roma kwa Babutale

Lisemwalo lipo. Said Fella amedai kuwa mstari aliorap Roma kwenye wimbo wake ‘Kaa Tayari’ ni maneno hata mtaani yapo yanazungumzwa kila siku.
fella-1[1]
“Bosi kamganda Dangote kaisahau Tip Top,” – amerap Roma kwenye wimbo huo.
Fella amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio kuwa mstari aliorap Roma ndani ya wimbo huo una ukweli ndani yake.
“Unajua Roma ni mtu mzima, alichoimba hata mtaani huko watu wanasema,
na unaweza kuona labda Roma ameambiwa hayo maneno na msanii kama Madee au msanii mwingine yeyote wa kwetu. Lakini hata mimi nilishawahi kumwambia mdogo wangu Babu Tale kuwa tufanye yote lakini yeye asiisahau
Tip Top Connection na mimi nisiisahau TMK,” amesema Fella.
Bado Tale hajajibu chochote kuhusiana na maneno hayo. Pamoja na kuwa meneja wa Tip Top, meneja huyo staa amekuwa akifanya kazi na Diamond na WCB nzima.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top