Baada ya kimya cha muda mrefu, mshindi wa tuzo za Africa Magic, Elizabeth ‘Lulu’ Michael, anakuja na filamu yake mpya iitwayo ‘Ni Noma.’
Filamu hiyo inaingia sokoni Ijumaa hii kwa mfumo wa dijitali ambapo watu watainunua na kuingalia kwenye smartphone zao kupitia app ya Proin Box.
Lulu ameiambia Bongo5 kuwa filamu hiyo imekuja na mapinduzi makubwa
kwa kila kitu kuanzia teknolojia na uigizaji. Amedai kuwa yeye na
kampuni yake ya Proin, walitaka kuja na kitu tofauti na vilivyozoeleka kwenye filamu za Tanzania.
“Ilitubidi kwa kiasi fulani tutulie, tusome mazingira, tasnia yetu inamiss nini sasa hivi, mashabiki wetu wanahitaji nini sasa hivi,” anasema Lulu
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )