Mwanamuziki Keisha baada ya kubanwa na masomo kwa muda
mrefu hali ambayo ilimfanya apate muda mchache wa kufanya muziki,
hatimaye anatarajia kumaliza masomo yake mwezi Disemba mwaka huu.
Muimbaji huyo ambaye pia mwaka jana alijikita kwenye siasa kwa kugombea nafasi ya ubunge wa viti maalum, mapema mwaka jana aliambia Bongo5 kuwa yupo mwaka wa pili katika chuo cha CBE na anachukuwa shahada
ya ununuzi na ugavi (Bachelor Degree in Procurement and Supplies Management).
Keisha ambaye ni mama wa watoto wawili, Jumatano hii amepost picha ya kitambulisho chake cha chuo na kuandika: Veryyyyy soon inshaAllah
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )