July 12 2016 Geah Habib alituletea hekaheka kutokea Tandale hospitali iliyokuwa ikimuhusu mgonjwa
aliyetoka nje ya hospitali na kukaa nje ya hospitali na akalala nje
usiku kucha, na mashuhuda siku hiyo walisema hospitali walipopewa
taarifa hawakujali. Mashuhuda walidai kuwa alishindwa kuhudumiwa kwa
sababu alikuwa hana shilingi 2000 ya kadi na mpaka anakata roho alikuwa
nje ya hosptali hiyo.
Sasa leo
July 18 2016 kupitia hekaheka ya Clouds FM, Geah Habib ametuletea
mwendelezo wa hekaheka baada ya kuwapata ndugu zake na Mganga mkuu wa
wilaya ambapo wameelezea ishu nzima ilivyokuwa, millardayo.com imekurekodia full stori kutoka kwenye HekaHeka ya leo.
Mganga mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Aziz Msuya amesema……..>>>’baada ya kuonana na madaktari walimshauri
kumpa dawa alikataa alikuwa na mwenza wake na wote wawili walikuwa
wamelewa, madaktari dawa ambazo walitaka kumpa ni zile ambazo haziwezi
kumdhuru hata kama alikuwa amelewa lakini kwa bahati mbaya alikataa’
>>>baada
ya kukataa kutibiwa pale walipewa barua ya rufaa yeye na mwenza wake
wakatoka nje ya geti wakawa wanasubiri usafiri, tungeweza kumpeleka na
ambulance lakini ilikuwa service, mwenzake alimuacha pale nafikiri
alimuambia amsubiri mwenzake ili waweze kwenda hospitali’:- Aziz Msuya
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )