Vijana wengi wanapofika umri fulani wa kupevuka kiakili hukumbwa na tatizo la chunusi kiasi ambacho huwakera na kuwakosesha raha kabisa.
Lakini siku ya leo sina lengo la kuzungumza kuhusu tatizo la chunusi leo nataka kueleza kuhusu yale mabaka meusi ambayo hubaki kwenye ngozi mara baada ya kuisha kwa chunusi.
Ni kweli kwamba yale mabaka meusi au kwa lugha ya wenzetu yaani kingereza hufahamika kama 'black spots' hukosesha raha kabisa na hata kupoteza muonekano wa muhusika pia.
Hapa ninazo baaadhi ya njia ambazo ukifanya husaida sana kuondosha
tatizo hilo la mabaka meusi yatokanayo na kupona kwa chunusi.
Juisi ya Limao
Hii juisi ni mojawapo ambayo huweza kuondosha mabaka kwenye ngozi
yako kutokana na juisi hii kuwa na kiwango kingi cha vitamin C ambayo
husaidia kufubaza yake madoa meusi kwenye ngozi yako.
Unachopaswa kufanya ili kutumia juisi hii ya limao kama tiba
utatakiwa kuandaa juisi hiyo ya limao kisha tafuta kipande cha pamba.
Baada ya kuandaa hivyo utachukua kipande cha pamba na kuchovya kwenye
juisi ya limao kisha utapaka moja kwa moja kwenye sehemu iliyoathirika
yaani sehemu yenye baka jeusi au mabaka meusi.
Baada ya kupaka juisi hiyo ya limao utakaa nayo kwa dakika kadhaa
kisha utaosha uso wako kwa maji safi na salama. Utaendelea kufanya hivyo
kwa muda wa wiki mbili mfululizo na utaanza kuona mabadiliko ya ngozi
yako.
Viazi Mviringo
Hivi viazi hutumika kwa kukata kata katika vipande vidogo vya
mviringo 'slice' kisha utaweka kipande hicho ile sehemu yenye tatizo
yaani yenye baka nyeusi na utaiacha hapo kwa muda wa dakika kadhaa kisha
utanawa kwa maji safi yenye umoto kiasi.Viazi mviringo |
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )