Kajala alitoa ushuhuda huo kwenye kipindi cha Friday Night Live ya (EATV) alipokuwa akiwapa hamasa mabinti na wasichana kutokukurupuka kwa kuangalia mali za wanaume bali wanapaswa kujisomea ili baadaye waje kuwa na maisha yao wenyewe, kwani yeye alikurupuka na kuolewa na matokeo yake aliishia kufungwa gerezani kwa sababu ya mwanaume wake.
"Ni kweli mfano mimi nilihongwa gari aina ya Harrier nikajikuta nakubaliana na mwanaume lakini baadaye nilikuja kujuta maana niliishia gerezani, hivyo nawaomba mabinti wenzangu tusikurupuke kwenye maamuzi, na wale wasichana ambao wanasoma wanapaswa kusoma ili baadaye waje kuwa na maisha ya kwao wenyewe" alisema Kajala
Kajala pamoja na wasanii wengine kama Mwasiti, Queen Darleen, Shilole wameanzisha kundi linalofahamika kama 'Sisters' ambacho lengo lake ni kutoa ushuhuda katika mambo mbalimbali ambayo yamewahi kuwatokea kwa wanafunzi wa kike wa shule za sekondari wakiwa na lengo la kuwahamasisha wanafunzi hao kusoma kwani maisha ambayo wao wamepitia hawataki wanafunzi hao nao waje kupitia.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )