Featured
Loading...

Utafiti: Watz Wengi Wameajiriwa Kwenye Ulinzi


Wanzania haiwezi kupiga hatua kimaendeleo na kupunguza tofauti ya hali ya maisha na kipato kwa watu wake iwapo idadi kubwa ya nguvu kazi ipo kwenye sekta ambazo hazina umuhimu mkubwa katika uzalishaji.


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa taasisi ya Society for International Development - SID ya nchini Canada na yenye ofisi zake jijini Nairobi nchini Kenya Bw. Arthur Muliro, amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa ripoti ya hali ya kipato kwa wakazi wa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki, ripoti iliyotolewa jijini Dar es Salaam hii leo.

Katika maelezo yake, Bw. Muliro amesema utafiti umeonyesha kwamba zaidi ya Watanzania milioni moja wameajiriwa kwenye sekta ya ulinzi na masuala ya usalama, idadi aliyodai kuwa ni tofauti na katika sekta nyingine muhimu kama za uhandisi na wataalamu ambao kwenye baadhi ya sekta idadi yao haizidi watu elfu kumi na sita.

Ameshauri kuwa juhudi kubwa zinahitajika kuongeza wataalamu kwenye sekta zilizoajiri watu wengi kama kilimo ambacho takribani asilimia themanini ya watanzania ndiyo wanayoitegemea kwa ajili ya kuendesha maisha yao.

Ripoti hiyo imetolewa na taasisi inalojihusisha na uboreshaji mazingira ya biashara, uchumi na uwekezaji kwa nchi za Afrika Mashariki ya Trade Mark East Africa ambapo SID ndiyo iliyofadhili utafiti huo uliohusisha nchi za Tanzania, Uganda, Rwanda, Kenya na Burundi.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top