Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaongeza dakika 4.
Dakika ya 86: Mohamed Ibrahim anaingia, anatoka Kichuya ambaye ndiye aliyefunga bao la Simba.
Dakika ya 84: Mchezo unaendelea kwa kasi pande zote.
Dakika ya 76: Azam wanafanya mabadiliko, anatoka Domayo anaingia Mudathir Yahya.
Dakika ya 74: Kapombe yupo chini, ameumia bega baada ya kukanyagwa naNdemla wakati wakiwania mpira, mchezo umesimama.
Dakika ya 73: Mavugo anaondoka na mpira, anapambana na mabeki wa Azam, anawapita, anatoa krosi ambayo Ndemla anashindwa kuitumia vizuri.
Dakika ya 67: KICHUYAAA GOOOOOOOOOO
Dakika ya 65: Simba wanafanya mashambulizi lakini moja kali linashindwa kutumiwa na washambuliaji wa Simba.
Dakika ya 64: Simba wanafanya mabadiliko, anatoka Mnyate anaingia Said Ndemla.
Dakika ya 60: Azam wanapata kona lakini inapigwa na inakuwa haina faida.
Dakika ya 55: Azam wanapanga mashambulizi taratibu, kocha wa Simba, Joseh Omog amesimama na anaonekana kuwa mkali kwa wachezaji wake.
Dakika ya 50: Timu zote zinashambuliana kwa zamu, beki wa Simba anavurugana na kiungo wa Azam Aboubakar Salum ‘Sure Boy’ lakini mwamuzi wanawaonya na mchezo unaendelea.
Dakika ya 46: Azam wanafanya shambulizi lakini mabeki wa Simba wanaokoa.
Kipindi cha pili kimeanza
Kipindi cha pili kimeanza
KIPINDI CHA KWANZA KIMEKAMILIKA
Mwamuzi anapuliza filimbi kukamilisha kipindi cha kwanza.
Dakika 45 + 2:Mchezo hauna kasi na unaweza kuwa mapumziko muda wowote kuanzia sasa.
Dakika ya 45; Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika mbili za nyongeza.
Dakika ya 43: Inapigwa faulo, Mavugo anaiunganisha kwa kichwa lakini Manula anadaka na wakati huohuo mwamuzi alikuwa ameshapuliza kipenga kuonyesha ameotea.
Dakika ya 42: Mnyate anafanyiwa faulo. Inaelekea kwenye lango la Azam.
Dakika ya 37: Azam wanacheza vizuri, wanapigiana pasi na kisha kupiga shuti lakinikipa wa Simba analidaka.
Dakika ya 33: Upande wa kushoto wa Simba kazi ni ngumu kati ya Kapombe na Mohammed Hussein ‘Zimbwe JR’ ambapo wote ni mabeki wa pembeni lakini wanakuwa wanapanda kusaidia mashambulizi, hivyo kunogesha ushindani wao.
Dakika ya 30: John Bocco wa Azam anapiga shuti kali langoni mwa Simba, kipa anatema kisha anadaka tena.
Dakika ya 28: Mnyate anaingia kwenye lango la Azam lakini mpira unatoka na kuwa goal kick.
Dakika ya 23: Ajib anabaki na kipa Aishi Manula lakini anakosa baada ya Manula kufanya kazi nzuri ya kuokoa hatari hiyo.
Dakika ya 20: Kiungo wa Azam, Migi anaonekana akipambana zaidi eneo la katikati.
Dakika ya 15: Simba wanakuwa wakali wanafanya mashambulizi kadhaa lakini Azam wanakuwa makini wanaokoa.
Dakika ya 7: Mchezo unachezwa zaidi katikati ya uwanja, Azam wamejaribu kufanya shambulizi lakini halikuwa na nguvu. Idadi ya mashabiki ni kubwa waliojotokeza uwanjani hapa.
Dakika ya 5: Mchezo bado haujawa na kasi, timu zote zinashambuliana kwa zamu.
Dakika ya 1: Mchezo umeanza hapa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
KIKOSI CHA SIMBA KILICHOANZA LEO HIKI HAPA:
1. Angban
2. Zimbwe Jr
3. Bokungu
4. Lufunga
5. Mwanjale
6. Mkude
7. Kichuya
8. Mzamiru
9. Mavugo
10. Ajib
11. Mnyate
Wanaoanzia benchi
Manyika
Ame Ali
Blagnon
Ndemla
Hamad
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )