Desemba 6, mwaka jana Mbongo
Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ alipata mtoto wa pili kupitia kwa mzazi
mwenzake, Zarina Hassan ‘Zari’ na kumpa jina la Nillan Nasibu ‘Chibu
Junior’, akiwa ametanguliwa na dada yake, Latifah ‘Tiffah’ aliyezaliwa
Agosti 6, 2015.
Kwa hesabu za harakaharaka, Januari 16,
mwaka huu, Nillan alikuwa anatimiza siku 40 tangu kuzaliwa kwake, lakini
siku hiyo imepita kavukavu huku wadau wake waliokaa mkao wa sherehe
wakibaki na maswali bila majibu.
SHUGHULI ILIKUWA KWENYE RATIBA
Wiki chache zilizopita, iliripotiwa
kwamba, Diamond kwa maana ya baba wa mtoto, aliandaa sherehe ya kufa mtu
ambayo ingefanyika jijini Johannesburg, Afrika Kusini ‘Sauzi’ ambako
mtoto huyo alizaliwa.
“Lakini kinachotushangaza wadau ni kwamba, mpaka siku zinakaribia hakuna dalili na matokeo yake, siku imepita hakuna lolote.
“Tulipewa kadi watu ambao tungekwenda
Afrika Kusini kwenye shughuli. Lakini naona kimya kingi mpaka Januari 16
imepita. Hakuna cha 40. Hata kama shughuli itafanyika Jumamosi hii
(keshokutwa) itakuwa si 40 tena, bali ni 45 sasa,” kilisema chanzo
hicho.
TOFAUTI NA TIFFAH
Baadhi ya wadau wa staa huyo sambamba na mashoga zake Zari waliliambia Amani kuwa, ujio wa Nillan hauna ‘vurugu’ kama ilivyokuwa kuzaliwa kwa Tiffah ambaye nchi ilisimama.
Siku ya 40 ya Tiffa
“Unajua huenda 4O ikawa imepoteza mvuto
baada ya ile ya Tiffah kuchukua nyota yote. Utakuwa unakumbuka mwandishi
kwamba, kuzaliwa kwa Tiffah Bongo ilitulia kimya. Hata siku ya 40 yake
kule nyumbani na baadaye kwenye ile shughuli ya Mlimani City, jina la
Tiffah lilikuwa juu sana.”
Siku ya 40 ya Tiffa
WENGI HAWAMJUI NILLAN
“Lakini sasa we fanya utafiti wa
kawaida tu, Wabongo wengi hawalijui jina la Nillan ambaye ni mdogo wake
Tiffah. Hakuna mbwembwe wala matangazo,” kilisema chanzo.
Prince Nillan Dangote
MABENKI YAMECHANGIA?
Habari zaidi zinasema kuwa, mbwembwe za
Tiffah mwaka juzi zilichangiwa na mabenki yaliyojitoa kumwaga pesa kwa
ajili ya kuchukua haki ya kwanza ya kumwonesha sura mtoto huyo ambapo
tofauti na ujio wa Nillan, hali ya mabenki imekuwa mbaya kiasi kwamba,
yale mawili yaliyotaka kuchukua haki hiyo yaliingia mitini.
“Ukifuatilia kwa karibu hapo utabaini
kuwa, kutojitokeza kwa mabenki hayo kumwaga pesa pia kumechangia
kudorora kwa vuguvugu la kuzaliwa kwa mtoto Nillan.
“Unajua hali ya uchumi ni mbaya kwa
sasa, nadhani hata Diamond mwenyewe anajiuliza kama akifanya sherehe
kubwa ya 40 halafu akatumia mfano milioni hamsini kama staa yeye
atafaidika na nini? Sherehe tu? Maana kama ni mtoto anaye tena ni wa
pili huyu.”
MAMA DIAMOND AREJEA BONGO, AJICHIMBIA MADALE
Awali ilidaiwa kuwa, baada ya mama
Diamond, Sanura Kasim ‘Sandra’ kwenda Sauzi kusubiria Zari kujifungua
Nillan, ratiba ilimtaka aendelee kutulia kulekule akisubiri 40 ambayo
ingefanyika kule lakini habari zinadai kutokana na kutokuwepo kwa ishu
hiyo, mwanamke huyo amerejea kimyakimya Bongo na amejichimbia Madale
nyumbani kwa mwanaye.
Diamond, mama Daimond kulia Rommie Jons
“Kama mnataka kujua kuwa 40 imebuma,
hata mama Diamond amerudi. Hivi ninavyoongea na wewe mwandishi, mama
amejaa tele Madale. Hakuna mbwembwe. Ama kweli hali ya uchumi wa mifuko
ni mbaya jamani,” kilisema chanzo.
ZARI NAYE ATUA BONGO
Habari zaidi za chini kwa chini zinasema
kuwa, mama Nillan, yaani Zari naye ametua Bongo bila mbwembwe hali
inayotoa taswira ya kutokuwepo kwa shughuli achilia mbali sherehe.
BABA DIAMOND AFUNGUA BEGI
Ikazidi kudaiwa kuwa, baada ya kuvunjika
kwa safari ya Sauzi, baba wa Diamond, mzee Abdul ambaye aliwahi
kuripotiwa kuwa, amekaa mkao wa safari, ilibidi afungue begi na kutoa
viwalo vyake kisha kuendelea na maisha yake ya kila siku, Bongo.
MADAI YACHUNGUZWA
Ilibidi Amani lishike
nyuzi hewani ili kuwasaka wahusika hao. Mtu mgumu sana kupatikana katika
wote ni Zari ambaye uchunguzi unaonesha kuwa, hata wale madansa wa
Diamond, akina Moses Iyobo hawana namba yake au wamepigwa marufuku kwa
kiapo kuigawa.
Hivyo Amani lilimtafuta Diamond mwenyewe kwa njia ya simu yake ya mkononi iliyoita weee mpaka ikakatika bila kupokelewa.
Amani likaona isiwe
shida, likamtumia meseji (SMS) kwa kuamini kwamba, kama alipopigiwa
alikuwa anaoga, anaendesha gari, anapafomu au yuko faragha, baada..
ya kuiona meseji hiyo angejibu lakini wapi!
MAMA DIAMOND
Ndipo Amani likamgeukia
mama Diamond mwenyewe ambaye ndiye anayetajwa kusimamia maandalizi ya
shughuli au kuamua kutosimamia kuandaa ambapo hali ilikuwa hivi:
Amani: (latoa utambulisho wa jina na chombo cha habari).
Mama Diamond: Aha! Niambie, unataka kunifundisha uandishi wa habari?
Amani: Ndiyo.
Mama Diamond: Haya nipe habari, nakusikiliza.
Amani: Napenda kujua,
kuna madai kwamba, shughuli ya 40 ya mdogo wake, Tiffah imeota mbawa,
hakuna. Je ni kweli au imeshafanyika kimyakimya?
Mama Diamond: (akakata simu).
Amani liliamini kuwa,
huenda simu hiyo imekatika kutokana na hali ya mtandao, likaacha
zikatika dakika kumi kwanza kabla ya kupiga tena.
Baada ya dakika kumi kupita…
Mama Diamond: We nani?
Amani: Mimi ni …(utambulisho wa jina na chombo cha habari).
Mama Diamond: (akakata simu).
BABA DIAMOND
Kwa upande wake, baba Diamond
alipotafutwa na kuulizwa kuhusu safari hiyo alisema yeye ni msikilizaji
kama safari ipo angekwenda kama haipo pia hana neno.
“Mimi ndugu yangu ni wa kusikiliza tu.
Kama safari ipo nakwenda, kama haipo hakuna neno. Kikubwa ni kumwomba
Mungu atupe uzima,” alisema.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )