Featured
Loading...

Kijana wa miaka 22 apandishwa kizimbani kwa Kosa la Kuua Kwa Kukusudia

Mkazi wa Ipililo wilaya ya Maswa Mkoani Shinyanga, Salum Nkoja (22) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Kisutu akikabiliwa na kosa la mauaji ya kukusudia ya mtu asiyefahamika.

Hata hivyo, kwa taarifa zilizoko inadaiwa mshtakiwa huyo alikamatwa na viungo vya binadamu zikiwemo sehemu za siri wanawake. Mshtakiwa alisomewa kosa lake na Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha ambapo amedai mshtakiwa anakabiliwa na kosa moja.

Katuga alidai mshtakiwa anakabiliwa na kosa la mauaji kwa kukusudia ambalo amelitenda kati ya October 1 na 30, 2017 katika sehemu isiyofahamika kati ya Ubungo Dar es Salaam na Kahama.

Wakili Katuga alieleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo anaomba kesi iahirishwe hadi tarehe nyingine.

Baada ya kusomewa kosa hilo, Hakimu Mkeha alimtaka mshtakiwa asijibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji, ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi December 8, 2017.

Katika taarifa zilizopatikana inadaiwa mshtakiwa huyo alikutwa na sehemu za siri za binadamu zilizokaushwa ambazo ni za wanawake.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top