Featured
Loading...

Waliofariki Fujo za Nairobi leo kumpokea Odinga ni Watu wawili


Kiongozi wa upinzani Kenya Raila Odinga leo amerejea nchini humo akitokea Marekani na kupokelewa na maelfu ya Wananchi kuanzia uwanja wa ndege.
Inaripotiwa kwamba fujo zimetokea baada ya Polisi kuingilia kati msafara huo ambapo zimesababisha vifo vya watu wawili huku Basi moja la Abiria (Matatu) likiteketezwa kwa moto pamoja na Lori moja la Polisi.
Mahakama ya juu nchini Kenya inatarajiwa kutoa uamuzi wake kuhusu uhalali wa Uchaguzi wa Tarehe 26 October ambapo Uhuru Kenyatta aliibuka mshindi huku Raila Odinga akiususia uchaguzi huo kwa kutoshiriki.  

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top