Wakati
zikiwa zimebaki siku 25 kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mdogo katika
Jimbo la Singida Kaskazini, kivuli cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo,
Lazaro Nyalandu kimeigawa Chadema katika pande mbili.
Wakati
Chadema taifa kikiwa kimeeleza kutoshiriki katika uchaguzi huo Januari
13 mwakani kwa madai ya kutokuridhishwa na uchaguzi wa udiwani wa Kata
43 uliofanyika Novemba 26, uongozi wa Chadema mkoa wa Singida jana
umempitisha mgombea atakayepeperusha bendera ya chama hicho.
Uchaguzi
wa jimbo hilo unafanyika baada ya Nyalandu kutangaza kujivua uanachama
wa CCM Oktoba 30 na kujiunga na Chadema huku mrithi wake akikigawa Chama
chake kipya cha Chadema.
Mwenyekiti
wa Chadema mkoa wa Singida, Shaban Limu amesema leo Desemba 19 kuwa
wamemteua Djumbe David Joseph kupeperusha bendera ya Chadema na
msimamizi wa uchaguzi wilaya ya Singida naye amempitisha.
“Leo
tunatarajia kufanya kikao cha kuweka mikakati ya kampeni. Kesho na
kesho kutwa, tutaingia kazini kwa kufanya kampeni zitakazokileta chama
matokeo tunayoyatarajia ambayo ni kushinda uchanguzi huo mdogo,” alisema
Limu
Mbali
na Djumbe, wagombea wengine na vyama vyao kwenye mabano ni Dalphina
Patrice Mlewa (CUF), Omari Mohammed Sombi (Alliance for Tanzania Farmers
Party), Monko Justein Joseph (CCM), Aloyce Mohammed Nduguta (Ada Tadea)
na Mchungaji Samwel Libisu (CCK).
Wagombea
hao walitangaza jana Desemba 18, 2017 na Msimamizi wa uchaguzi wilaya
ya Singida, Rashid Mandoa amesema wamepitisha wagombea hao baada ya
kukidhi vigezo vyote vinavyo hitajika.
Mandoa
amesema wagombea kutoka vyama vya NRC na UMD wao hawakupitishwa baada
ya kushindwa kukidhi vigezo. Pia wagombea kutoka UDP na UDPP
hawakurudisha fomu.
Akizungumzia
uamuzi huo, Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa
Chadema, John Mrema amesema; ‘’kwa mjibu wa Katiba ya Chadema, Kamati
Kuu ndiyo inayopitisha jina la mgombea na Kamati Kuu haijakutana sasa
hilo jina limepatikanaje.”
“Tutashangaa
hata NEC (Tume ya Taifa ya Uchaguzi) kama wataendeleza mchakato wa jina
hilo na tumeagiza tuletewe taarifa na hatua zitachukuliwa kwa wahusika
kwani kilichofanyika ni kosa la jinai, kama barua ya Katibu Mkuu
kuthibitisha kupitishwa na Chama haipo wao wameitoa wapi,” amehoji Mrema
Amesema
kama kuna watu wametumiwa basi watambue kwamba msimamo wa chama
haujabadilika na wanafuatilia suala hilo na hatua zitachukuliwa kwa
viongozi waliohusika.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )