Dkt.
Louis Shika ambaye amejizolea umaarufu baada ya kuibuka mshindi katika
mnada wa nyumba za mfanyabiashara maarufu, Said Lugumi, na kushindwa
kuzilipia, ameandaliwa usiku wake maalum ambao ataongea na Watanzania
juu ya maisha yake.
Akizungumza
na waandishi wa Habari mapema jana Novemba 30, 2017, Jijini Dar es
Salaam, Meneja wa Dkt. Shika, Catherine Kahabi aliweka wazi kuwa
wamekuja na wazo hilo la kuandaa tamasha maalum ili watu wote wamtambue
Dkt. Shika kama mmoja wa watu wakubwa ambao wameweza kuibuka katika
mazingira ya chini na baadae kuwa gumzo kila kona.
“Usiku
wa 900 Itapendeza ni usiku maalum ambao unatarajiwa kufanyika Desemba
9, mwaka huu. Watu wote wanakaribishwa pale ndani ya uwanja wa burudani,
Dar live. Usiku huo ni maalum na Dkt. Shika ataweka wazi kila kitu
pamoja na historia yake alianzia wapi mpaka kufika Nchini Urusi na
baadae kurejea Tanzania” amesema Catherine
Pia
aliongeza kuwa, kwa sasa wanamuangalia Dkt. Shika kama ni mmoja wa
Watanzania wenye bahati na muonekano wa tofauti licha ya kila mmoja
kusema lake.
Mbali
na Dkt. Shika, kutakuwa na burudani mbalimbali zitakazosindikizwa na
bendi ya Twanga Pepeta, Jahazi Modern Taarab na wasanii wengine kibao
wakiwemo wa Bongo fleva na wachekeshaji akiwemo MC Pilipili.
Kwa
upande wake msimamizi wa masuala ya burudani wa Dar Live, Rajabu Mteta
(KP Mjomba) amesemakuwa usiku huo utapambwa na shamrashamra mbalimbali
kwani utakuwa ni wa aina yake kwa kila mmoja atakayefika siku hiyo.
“Wengi
bado wapo njia panda kuhusiana na ukweli wa mabilioni ya Dkt. Shika,
tumeshuhudia hivi karibuni amelipia bima fedha zilizopo nje ya nchi.
Kabla fedha hizo hazijatua ameona awashangaze wananchi ambapo ukija Dar
Live utaishuhudia,” amesema Mteta KP Mjomba.
Usiku
huo pia unatarajiwa kuwa na mgeni rasmi ambaye atafungua halfa hiyo,
Mkurugenzi wa Global Group, Erick Shigongo kama mtu aliyemsaidia kwa
namna moja ama nyingine Dkt. Shika.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )