Kituo
cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeitaka serikali kufanya
uchunguzi wa kina sambamba na kuchukulia hatua kali za kisheria, kwa
watakao bainika kuhusika na uvunjifu wa haki za binadamu katika uchaguzi
mdogo wa madiwani wa marudio wa Novemba 26, 2017 uliofanyika katika
kata 43.
Akizungumza
na wanahabari jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
LHRC, Anna Henga amesema Kituo hicho kilifuatilis kwa ukaribu uchaguzi
huo, na kubainj uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu na taratibu za
uchaguzu nchini licha ya kuwa wa huru na haki.
“Kumekuwa
na vitendo vya matumizi mabaya ya nguvu ya vyombo vya dola, matukio ya
watu kutekwa na wasiojulikana, watu kupigwa, kukamatwa na kujeruhiwa kwa
lengo la kuharibu na kuvuruga uchaguzi na kuwatia hofu wapiga kura.
Vitendo hivi vimeripotiwa kufanywa na vyombo vya dola, watu
wasiojulikana na wanaosadikiwa kuwa wafuasi wa vyama vya siasa ikiwemo
CCM na Chadema,” alisema.
Henga
alisema LHRC inatahadharisha kwamba matukio hayo yasipokemewa na jamii
in kiashiria kibaya na msingi mbaha utakao athiri chaguzi zijazo ikiwemo
wa serikali za mitaa wa mwaka 2019 na Mkuu wa 2020.
“Hii
itapelekea kutishwa wapiga kura wasijitokeze kutekeleza haki zao za
msingi za kuchagua viongozi wao, kuchochea uhasama miongoni mwa wananchi
pamoja na kufifisha imani ya wananchi juu ya vyombo vys usimamizi wa
uchaguzu na dola kwa ujumla,” alisema.
Kwa
upande wake Mwanasheria wa LHRC, William Benjamin ameitaka serikali
kufanya maandalizi ya kimfumo, kikatiba na kisera ili iweze kudhibiti
vitendo vitakavyoweza kuharibu uchaguzi.
“Tunashauri
mchakato wa katiba urejewe, kuwepo tume huru ya uchaguzi. Vyombo vya
dola vijue kazi yake ni kulinda wananchi wanapokuwa kwenye uchaguzi na
si kuvuruga uchaguzi,” alisema.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )