1.0. UTANGULIZI
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Katika kipindi hiki, Serikali imeendelea kutekeleza changamoto zinazowakabili wananchi kwa kuweka sera madhubuti zinazosaidia kutatua changamoto mbalimbali ambazo Mhe. Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitoa mwelekeo wake wakati akifungua Bunge jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 20 Novemba, 2015 hapa Dodoma.
Baada ya maelekezo haya, hatua kadhaa zimechukuliwa na mafanikio dhahiri tumeanza kuyaona.
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Mafanikio
dhahiri yameanza kuonekana katika kipindi hiki kifupi. Mafanikio
yaliyopatikana ni pamoja na kuimarika kwa nidhamu kwa Watumishi wa Umma;
mabadiliko ya hali ya uchumi; kutekelezwa kwa miradi ya maendeleo;
kuongezeka kwa mapato ya ndani; kupungua kwa rushwa, kuimarika kwa
Muungano wetu na kushughulikiwa kwa migogoro ya ardhi.
Suala la Nidhamu, Rushwa na Dawa za Kulevya.
Serikali
iliweka dhamira ya kuwahudumia wananchi wote hususan maskini kwa
kuwapelekea miradi ya maendeleo na huduma muhimu za jamii. Ili kufikia
azma hii ilibidi tuanze kujenga nidhamu ya Watumishi wa Umma kwa kubaini
wazembe, wabadhilifu, wezi wa mali na fedha za umma, wala rushwa mahali
pa kazi na wasio tayari kuwatumikia wananchi na hasa wanyonge; na
kusimamia mwenendo wa uchumi kwa kuongeza uzalishaji mali na kukusanya
mapato.
Tulianzisha
mapambano ya wazi dhidi ya vitendo vya rushwa na ufisadi pamoja na
mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya. Yote haya ilikuwa ni
mkakati wa kuwezesha kutekeleza Ilani yetu kwa vitendo na kwa mafanikio.
Yote haya tumeyaeleza kwa kirefu kwenye vitabu tulivyowapa.
2.0. HALI YA UCHUMI
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Mwenendo
wa viashiria vya ukuaji wa uchumi wa Nchi yetu kwa mwaka 2016 na 2017
vinaonesha kuwa uchumi wetu unakua na kuimarika. Kwa mujibu wa takwimu
zilizotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, ukuaji halisi wa Pato la
Taifa kwa mwaka 2015 na 2016 ulikuwa asilimia saba na hivyo kuifanya
Nchi yetu kushika nafasi ya tatu kwa ukuaji wa uchumi barani Afrika.
Tafiti na uzoefu kutoka nchi zilizoendelea unaonyesha kwamba, mwenendo
huu wa ukuaji wa uchumi utaiwezesha Tanzania kufikia kundi la Nchi zenye
Uchumi wa Kati lenye wastani kipato cha Dola za Marekani 1,043 sawa na
wastani wa Shilingi Milioni 2.4 kwa mwaka. Wastani wa Pato la Mtanzania
umeongezeka kutoka Shilingi Milioni 1.9 kwa mwaka 2015 hadi kufikia
Shilingi Milioni 2.1 mwaka 2016, sawa na ongezeko la asilimia 11.
Aidha,
Serikali imeweka juhudi kubwa katika ukusanyaji wa mapato. Kutokana na
juhudi hizo, makusanyo ya ndani kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
yaliongezeka kutoka wastani wa Shilingi Bilioni 850 kwa Mwezi mwaka
2015 hadi Shilingi Trilioni 1.3 kwa Mwezi mwaka 2017 sawa na ongezeko la
asilimia 34.6.
Kupitia
makusanyo hayo sasa serikali inaendelea kupeleka fedha za miradi ya
maendeleo katika kila Halmashauri, Idara za Serikali, Wizara kwa kiasi
cha Shilingi bilioni 428.5 kila mwezi.
(Sekta ya Uchumi na Fedha imeelezwa kwa kina kuanzia ukurasa wa 4 hadi wa 8 wa vitabu mlivyogawiwa).
3.0. SEKTA ZA UZALISHAJI
3.1. KILIMO
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Ilani
ya Chama cha Mapinduzi imeielekeza Serikali kutilia mkazo kuendeleza
sekta ya kilimo ili kukifanya kilimo kuwa cha kisasa, chenye tija na cha
kibiashara ambacho mazao yake yaongezwe thamani. Serikali imeimarisha
upatikanaji wa pembejeo na zana za kilimo, kuimarisha huduma za ugani,
kuimarisha huduma za umwagiliaji, kuwezesha upatikanaji wa masoko na
kuhamasisha Sekta binafsi, vyama vya ushirika na kanzisha viwanda vya
kusindika mazao ya kilimo.
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Katika
kipindi cha mwaka 2016/2017 Serikali iliingia makubaliano na kampuni za
kuzalisha na kuuza mbegu kwa bei ambayo ni rahisi kwa mkulima. Serikali
pia imeanzisha mfumo mpya wa ununuzi wa mbolea ambapo kwa sasa ununuzi
wa mbolea hufanywa kwa pamoja. Mfumo huu unaongeza upatikanaji wa mbolea
na unapunguza bei kwa asilimia 30 kwa mkulima, mfuko wa mbolea sasa
unauzwa kati ya Shilingi 50,000/= hadi 60,000/= na mfumo huo umeanza
msimu huu wa kilimo ambapo hadi Septemba 2017 jumla ya tani 55,000
zimeingizwa nchini. Tayari manufaa yake tumeanza kuyaona.
Serikali
inaendelea kuhimiza Bodi za mazao ya pamba, korosho, kahawa, ufuta,
tumbaku na mazao mengine kuandaa mbegu na madawa ya kuulia wadudu kwa
haraka na bei nafuu.
Kwa
upande wa zana za kilimo, Serikali imejenga uwezo wa sekta binafsi
katika kuwezesha upatikanaji wa zana za kilimo ambapo katika kipindi cha
Novemba 2016 na Septemba 2017 jumla ya matrekta makubwa 2,500 na
matrekta ya mkono 336 yaliingizwa nchini na sekta binafsi. Kupitia
mpango wa kuendeleza viwanda, Tanzania imeanza kuunganisha matrekta ya
kilimo kupitia kampuni ya Ursus ambayo tayari imetengeneza matrekta 1894
ya ukubwa tofauti. Pia, Serikali imenunua mashine za kisasa 14 za
kusindika mpunga zenye uwezo wa kukoboa kati ya tani 5 hadi 30 kwa siku
kwenye skimu 13 za umwagiliaji nchini.
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali
imeongeza Maafisa Ugani kutoka 9,558 mwaka 2015 hadi 13,532 mwaka 2017.
Kati ya hao, 8,232 ni Maafisa Ugani wa sekta ya kilimo, 4,283 mifugo,
493 uvuvi na 524 ni Maafisa Ushirika. Vituo vya mafunzo ya kilimo na
mifugo vya kata vimeongezeka kutoka 147 mwaka 2015 hadi 322 kufikia
Juni, 2017, sawa na ongezeko la asilimia 54.3 kwa sekta zote.
Aidha,
Serikali imejenga masoko na maghala ya kimkakati katika mipaka ili
kudhibiti wafanyabiashara kutoka nje ya Nchi kuingia moja kwa moja
mashambani na kununua mazao ya wakulima kwa bei ndogo. Aidha, mfumo wa
stakabadhi ghalani umeonyesha mafanikio makubwa na mabadiliko ya Uongozi
kwenye Menejimenti ya Bodi umeonesha matokeo chanya katika zao la
korosho. Mfano, katika msimu wa 2015/2017 kiasi cha korosho kilo laki
moja na hamsini na tano (155,244,645) ziliuzwa kwa bei ya Shilingi
Bilioni mia tatu themanini na nane (388,474,530,906.40). Mheshimiwa
Rais baada ya kutoa pembejeo bure kwa wakulima, uzalishaji umeongezeka
na mwaka huu 2017/2018 hadi kufikia sasa kilo laki mbili sitini na tano
(265,651,031) zimeuzwa kwa thamani ya Shilingi Trilioni moja nukta moja.
Ambapo inatazamiwa kuwa hadi mwisho wa msimu itafikia 300,000 tutapata
sio chini ya trilioni 1.4. Wastani wa bei kwa kilo umepanda kutoka
Shilingi 1,300 hadi Shilingi 4,000.
(Mafanikio tuliyoyapata katika Sekta ya Kilimo yameelezwa kwa kina kuanzia ukurasa wa 8 hadi wa 13 wa vitabu mlivyogawiwa).
3.2. MIFUGO
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Kwa
upande wa sekta ya mifugo Serikali inaongeza uzalishaji wa mitamba,
kujenga miundombinu ya mifugo ikiwemo malambo na mabwawa, kuzalisha
mashamba darasa ya malisho, kuendeleza na kutoa elimu ya teknolojia ya
uhamilishaji, kutenga, kupima na kumilikisha wafugaji maeneo ya ufugaji.
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Katika
kutekeleza maelekezo haya ya Ilani, Serikali inatoa elimu kwa wafugaji
kufuga mifugo itakayompa tija mfugaji. Tumeanza kutambua mifugo kwa
kuweka alama, kujua idadi na mahali ilipo ili kuweka takwimu, tumeagiza
Maafisa Mifugo kuhudumia mifugo, tumezuia mifugo kutoka nje ili
kuondokana na migogoro ya wafugaji na wakulima, magonjwa, n.k. tumetenga
maeneo ya mifugo kila wilaya na mikoa. Hadi sasa, tumetenga jumla ya
hekta 519,918 za maeneo ya ufugaji kwenye vijiji 80 katika Wilaya 17 za
Mikoa 11 ya Tanzania Bara na kufanya jumla ya eneo lililotengwa hadi
sasa kufikia hekta milioni 2.535 katika vijiji 728. Aidha, jumla ya hati
za kumiliki ardhi kimila 44 zimetolewa kwa wafugaji katika Wilaya za
Monduli, Ngorongoro, Hanang, Simanjiro na Karatu. Pia, Serikali
imeanzisha mashamba darasa ya uzalishaji malisho katika Halmashauri za
Bunda, Busega, Kiteto na Igunga. Lengo ni kuanzisha mashamba darasa
katika maeneo yote ya wafugaji nchini.
Tumetoa
mafunzo ya uhamilishaji kwa wahamilishaji 264 yanayohusu mabadiliko ya
teknolojia, tumetoa vitendea kazi, ukarabati wa miundombinu, mitambo ili
huduma za uhamilishaji ziwe za uhakika.
Pia, tunahamasisha ujenzi wa viwanda vya kuchakata mazao ya mifugo ili kumpatia faida kubwa mfugaji.
(Mafanikio tuliyoyapata katika Sekta ya Mifugo yameelezwa kwa kina kuanzia ukurasa wa 14 hadi wa 18 wa vitabu mlivyogawiwa).
3.3 USHIRIKA
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali
inaendelea kusimamia sekta ya ushirika ambayo ilikuwa imepoteza
mwelekeo. Dhana ya ushirika ni nzuri na endapo itasimamiwa vizuri,
itamnufaisha mkulima. Serikali imeanza kuchukua hatua mbalimbali za
kufufua ushirika nchini kwa kufanya uhakiki wa mali na kusimamia fedha
za ushirika.
Mheshimiwa
Rais ameunda Tume ya Ushirika, tunaunda ushirika kwenye mazao
yanayoendesha ushirika, tunachukua hatua kwa viongozi wanaofuja mali na
fedha za ushirika, tulianza na ushirika wa korosho, tumbaku, chai.
Uchunguzi unafanywa kwa ushirika wa Kahawa. Tutaendelea na hatua hizo
kwa mazao yote yanayoendeshwa kwa ushirika. Serikali inataka kuona
Maafisa Ushirika wanasimamia ushirika ili mkulima mnyonge anufaike na
kilimo kupitia ushirika.
3.4 MALIASILI NA UTALII
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Utalii
ni moja ya sekta zinazochangia kwa kiasi kikubwa katika Pato la Taifa
na ajira kwa wananchi. Kwa kutambua umuhimu wa sekta hiyo Serikali
inasimamia utekelezaji wa mikakati ya kukuza utalii nchini kwa
kuhakikisha idadi ya watalii inaongezeka, kuongeza bajeti ya sekta ya
utalii, kuimarisha mafunzo ya utalii, kujenga mazingira ya kuwezesha
vijana kuanzisha makampuni ya kitalii na kuhifadhi malikale. Pia
tunatatua migogoro ya mipaka kati ya wananchi na mapori yaliyohifadhiwa
kwa lengo la utalii.
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali
imeendelea kuboresha miundombinu ya utalii ikiwemo kukarabati kilometa
2,571 za barabara zilizopo ndani ya hifadhi, njia za miguu zenye urefu
wa kilometa 143.5 na kuongeza matangazo ya utalii ndani na nje ya Nchi.
Juhudi hizo zimewezesha idadi ya watalii kuongezeka kutoka 1,137,182
mwaka 2015 hadi 1,284,279 mwaka 2016, sawa na ongezeko la asilimia 12 na
kuliingizia Taifa Dola za Marekani Bilioni 2. Aidha, katika mwaka wa
fedha 2017/2018 Serikali imeongeza bajeti ya utalii hadi kufikia
Shilingi Bilioni 6.6 ikilinganishwa na Shilingi Bilioni 4.2 zilizotengwa
mwaka 2016/2017. Tunaimarisha matangazo ya vivutio vya Kitalii ili
kuongeza idadi ya Watalii.
Serikali
imehakiki mipaka yote ya maeneo ya hifadhi ikiwemo Ngorongoro kwa
kuweka alama za kudumu na mabango ya tahadhari. Hadi mwezi Mei, 2017
vigingi 14,755 vimesimikwa, sawa na aslimia 62.4 ya vigingi 23,638
vinavyohitajika. Serikali inaendelea kudhibiti ujangili na uharibifu wa
Misitu ili kulinda maliasili zetu.
(Mafanikio
tuliyoyapata katika Sekta ya Maliasili na Utalii yameelezwa kwa kina
kuanzia ukurasa wa 19 hadi wa 23 wa vitabu mlivyogawiwa).
3.5 VIWANDA
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali
inahakikisha kuwa uchumi wa Nchi yetu unakua kwa kuifanya Tanzania kuwa
Nchi ya viwanda. Katika kujenga uchumi wa viwanda, Serikali
imehamasisha wawekezaji wa ndani na nje kujenga viwanda vidogo, vya kati
na vikubwa. Viwanda vinavyopewa kipaumbele ni vile vinavyotumia
malighafi zinazopatikana hapa nchini, vinavyotoa ajira kwa watu wengi na
vinavyozalisha bidhaa zenye soko hapa ndani na nje ya Nchi.
Tumeona
mwitikio mkubwa wa sekta binafsi kuwekeza katika viwanda. Baadhi ya
viwanda vilivyoanzishwa katika kipindi cha kuanzia Novemba, 2015 ni
pamoja na; kiwanda cha kusindika maziwa cha Milkcom Ltd kilichopo
Kigamboni – Dar-es-Salaam ambacho uwekezaji wake ni Shilingi Bilioni 44
na kina uwezo wa kuzalisha lita milioni 67.5 za maziwa kwa mwaka na
kutoa ajira kwa watu 500; kiwanda cha nyama cha Meat King Ltd kilichopo
eneo la Moshono – Mkoa wa Arusha kimewekeza Shilingi Bilioni 5.5 kwa
ajili ya kusindika nyama ya ng’ombe, kuku na kondoo; kiwanda cha Lakairo
Polybag kilichopo Mwanza ambacho uwekezaji wake ni Shilingi Bilioni 4
chenye uwezo wa kuzalisha magunia ya sandarusi milioni 10 kwa mwaka;
kiwanda cha Global Packaging kilichopo Kibaha – Pwani kimewekeza
Shilingi Bilioni 8 chenye uwezo wa kuzalisha magunia ya sandarusi
milioni 11.75 kwa mwaka na ajira ya watu 110. Kiwanda cha Nyama
kilichopo hapa Dodoma kinachinja Ng’ombe 350 – 500 kwa siku.
Baadhi
ya viwanda vikubwa vinavyoendelea kujengwa hapa nchini ni: Kilua Steel
Group – kiwanda cha nondo kinazalisha tani 2000 kwa siku; kiwanda cha
marumaru cha Goodwill kilichopo Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani; kiwanda
cha kusokota nyuzi za pamba cha NAMERA kilichopo Gongolamboto,
Dar-es-Salaam; kiwanda cha kukausha mbogamboga cha Vegeta Padravka Ltd
kilichopo Bagamoyo – Pwani ambacho uwekezaji wake unatarajiwa kuwa
Shilingi Bilioni 9.9 na kiwanda cha kusindika nyama cha Nguru Hills
Ranch kinachojengwa Mvomero – Morogoro ambacho kitahitaji ng’ombe 50,000
na mbuzi 60,000 kwa mwaka.
Serikali inaweka mkazo wa ujenzi wa viwanda, kila Mkoa ili kuzalisha bidhaa pia kupunguza tatizo la ajira nchini.
(Mafanikio tuliyoyapata katika Sekta ya Viwanda yameelezwa kwa kina kuanzia ukurasa wa 24 hadi wa 26 wa vitabu mlivyogawiwa).
3.6 MADINI
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Ili
kuhakikisha Sekta ya Madini inachangia kikamilifu katika kukuza uchumi
na ajira, Serikali inaimarisha ukaguzi wa uzalishaji na mauzo ya madini
katika migodi mikubwa na midogo nchini ambapo katika kipindi cha
Novemba, 2015 hadi Novemba, 2017 jumla ya sampuli 8,497 za mikuo ya
dhahabu na makinikia ya shaba (copper concentrate) kutoka kwenye migodi
mikubwa zilifanyiwa uchunguzi kwenye maabara ili kujua kiasi na thamani
ya madini yaliyozalishwa na kuuzwa nje. Kaguzi pia zilifanywa katika
Migodi ya Tanzanite One na Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Ngaka ambazo
zimeiwezesha Serikali kukusanya mrabaha wa jumla ya Dola za Marekani
Milioni 6.99. Aidha, Serikali imefanya ukaguzi katika uzalishaji na
mauzo ya madini ya ujenzi na viwandani katika Mikoa mbalimbali chini na
kuwezesha malipo ya mrabaha wa Shilingi Bilioni 9.97. Mrabaha huo
unatokana na uzalishaji na mauzo ya tani milioni 20.69 za madini ya
ujenzi na viwandani yenye thamani ya Shilingi Bilioni 324. Kwa sasa
tunaendelea na ujenzi wa ukuta wa eneo la Tanzanite ili kudhibiti
utoroshaji.
Vilevile,
ukaguzi wa shughuli za uzalishaji na mauzo ya dhahabu kutoka kwa
wazalishaji wanaotumia teknolojia ya “vat leaching” kuchenjua marudio
katika Mikoa ya Mbeya, Mwanza, Geita, Shinyanga na Tabora umefanyika.
Jumla ya kilo 2,500 za dhahabu zenye thamani ya Shilingi Bilioni 183
zilizalishwa na wamiliki halali wa leseni katika maeneo hayo. Ukaguzi
huo umewezesha malipo ya mrabaha wa kiasi cha Shilingi Bilioni 7.3.
Ukaguzi umefanyika pia kwa Wachimbaji Wadogo wa dhahabu katika Wilaya za
Chunya, Geita na Mpanda ambapo jumla ya Kilogramu 48.68 za dhahabu na
mifuko 100,287 ya mawe yenye madini ya dhahabu yenye thamani ya wastani
wa Shilingi Bilioni 6 ilizalishwa na wachimbaji hao na fedha Shilingi
Milioni 244 zilikusanywa kama mrabaha. Mapato haya ni sehemu tu ya fedha
zinazopatikana, nyingi zinapotea kwa utoroshaji wa madini yetu.
Katika
jitihada za kulinda rasilimali za Taifa ikiwemo Rasilimali za Madini,
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Mwenyekiti wa CCM aliagiza kuundwa kwa Tume mbili maalum za
uchunguzi wa makontena yaliyokuwa na mchanga wa makinikia yaliyokamatwa
bandarini, Dar-es-Salaam, na maeneo mbalimbali nchini na kuagiza kupata
taarifa za uchunguzi huo. Aidha, Mheshimiwa Rais alizuia usafirishaji wa
makinikia nje ya Nchi baada ya kugundua wizi wa utoroshaji unaofanywa
na baadhi ya makampuni makubwa. Serikali ilitoa waraka wa sheria Bungeni
wa kutunga Sheria ya Kulinda Rasilimali za Nchi. Tulikamata makontena
yapatayo 423 yenye makinikia yaliyokuwa yanatoroshwa kwenda nje ya Nchi.
Serikali
imehamasisha wawekezaji wa Smelter na Refinery kujitokeza kwa ajili ya
kujenga mitambo hiyo hapa nchini. Jumla ya kampuni 25 zimeonesha nia na
Serikali inaendelea na utaratibu wa kutafuta kampuni zitakazofaa kwa
ajili ya ujenzi wa mitambo hiyo. Vilevile, Serikali itaendelea
kuisimamia na kuilinda sekta ya madini na itaendelea kujiridhisha kuwa
Watanzania wananufaika vizuri.
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali
katika kipindi cha Novemba, 2015 hadi Julai, 2017 imetoa jumla ya
leseni 4,207 zenye ukubwa wa kilomita za mraba 74.1 zimetolewa kwa
wachimbaji wadogo wa madini kote nchini. Aidha, jumla ya maeneo 11 yenye
ukubwa wa hekta takribani 38,951 yenye uwezo wa kutoa leseni za
uchimbaji 3,895 yametengwa kwa ajili ya wachimbaji wadogo katika Mikoa
ya Kagera, Singida, Katavi, Ruvuma, Lindi, Tabora na Geita. Pia,
Serikali imetoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo 2,000 kuhusu teknolojia
mbadala za uchenjuaji dhahabu, usalama migodini, ujasiriamali, utunzaji
kumbukumbu na utunzaji wa mazingira.
(Mafanikio tuliyoyapata katika Sekta ya Madini yameelezwa kwa kina kuanzia ukurasa wa 26 hadi wa 32 wa vitabu mlivyogawiwa).
4.0.SEKTA YA MIUNDOMBINU NA HUDUMA ZA KIUCHUMI
4.1. ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali
inatekeleza mipango ya kuendeleza ardhi ikiwa ni pamoja na kujenga
mfumo utakaorahisisha umilikishaji wa ardhi na uhifadhi wa kumbukumbu za
ardhi kwa kukamilisha ujenzi wa Mfumo Unganishi wa Kuhifadhi Kumbukumbu
za Ardhi, kutekeleza Mpango wa Taifa wa Matumizi ya Ardhi, kutatua
migogoro, kero ya ardhi kote nchini na kuhakikisha kuwa kila mwenye
ardhi anapimiwa na kupewa hati.
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali
imeanza kufunga Mfumo unganishi katika Halmashauri za Manispaa za
Kinondoni na Ubungo Jijini Dar-es-Salaam. Kazi hiyo inatarajiwa
kukamilika Juni, 2018 na baadaye Mfumo huo utafungwa katika Halmashauri
zote nchini. Aidha, Serikali imeboresha Mfumo wa Ukusanyaji Kodi ya
Pango la Ardhi kwa kuweka Mfumo maalumu uitwao Government e-payment
Gateway System katika Halmashauri 31 na hivyo kukomesha vitendo vya
Maafisa Ardhi kugawa viwanja mara mbili; na sasa ada na tozo zote
kulipwa kwa njia ya kielektroniki pia simu za mkononi. Serikali imeunda
Bodi ya Mfuko wa Fidia ya Ardhi yenye jukumu la kufuatilia na kuratibu
malipo yote ya fidia yatakayofanywa na Wizara, Idara za Serikali
zinazojitegemea, Wakala, Mikoa na Halmashauri. Mwongozo wa namna
shughuli za Mfuko wa Fidia ya Ardhi zitakavyofanyika umeandaliwa na
kusambaza kwa wadau.
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali
imefanya uhakiki wa mashamba pori yasiyoendelezwa ambapo ukaguzi wa
mashamba ya uwekezaji 121 yenye ukubwa wa ekari 552,139 katika Mikoa ya
Tanga, Morogoro, Dar-es-Salaam, Lindi, Manyara, Arusha Pwani, Njombe na
Kagera umefanyika ambapo mashamba 58 yalibainika kutoendelezwa. Mashamba
hayo pamoja na mengine yenye ukubwa wa ekari 429,654 yaliyopo katika
Mikoa ya Tanga, Pwani, Kilimanjaro, Morogoro, Iringa na Dar-es-Salaam
yamefutiwa umiliki na kurudishwa kwa halmashauri husika kwa ajili ya
kuandaliwa mipango ya matumizi ya ardhi na kuigawa kwa kuzingatia
mahitaji ya ardhi yaliyopo katika eneo husika. Tutaendelea kubaini
mashamba makubwa ambayo hayajaendelezwa na kuyagawa kwa wananchi.
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali
imepima vijiji 11,000 kati ya vijiji 12,545 Nchi nzima hadi kufikia
Agosti, 2017. Pia, jumla ya hatimilki za kimila 69,208 zimeandaliwa na
kutolewa kwa wananchi katika maeneo mbalimbali nchini. Kwa upande wa
upimaji wa viwanja, jumla ya hatimiliki za viwanja 82,633 na nyaraka za
kisheria 122,106 zimesajiliwa na kutolewa. Kazi ya kubainisha viwanja
50,200 vitakavyorasimishwa katika Halmashauri za Manispaa za Musoma,
Kigoma Ujiji, Tabora, Singida, Sumbawanga na Lindi inaendelea.
(Mafanikio
tuliyoyapata katika Sekta ya Ardhí, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
yameelezwa kwa kina kuanzia ukurasa wa 32 hadi wa 40 wa vitabu
mlivyogawiwa).
4.2. UJENZI NA UCHUKUZI
4.2.1. Barabara
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali
inaendelea kujenga miradi ya barabara na madaraja kwa kuzingatia
vipaumbele kama ilivyoainishwa katika Ilani ya Chama chetu. Ili kuongeza
ufanisi katika kutekeleza miradi ya barabara mijini na vijijini,
Serikali imeanzisha Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini -TARURA
yenye jukumu la kusimamia kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara za
mijini na vijijini ambazo ziko chini ya TAMISEMI ambazo hazipo chini ya
Wakala wa Barabara Kuu yaani TANROADS.
Aidha,
Serikali imeendelea kukamilisha kujenga barabara Nchi nzima. Zipo
zilizokamilimika kwa kuunganisha Mikoa na miradi mbalimbali inatekelezwa
kwa kiwango cha lami. Hii ni kukamilisha ndoto ya Mheshimiwa Rais ya
kuwa Watanzania watasafiri kwa gari aina ya Mark II kutoka Sirari
wilayani Tarime mkoani Mara hadi Mbamba Bay – Ruvuma, kwa kupita juu ya
barabara ya lami.
Mpaka
sasa tumekamilisha na tunaendelea na ujenzi wa barabara zenye urefu wa
zaidi ya kilomita 1,500 kwa zaidi ya Shilingi trilioni 1.8 zikiwemo
Barabara za:
(i) Dodoma – Kondoa – Babati Km. 232; Shilingi Bilioni 335.46
(ii) Tunduma – Sumbawanga Km. 223; Shilingi Bilioni 350.2
(iii) Tunduru- Nakapanya- Mangaka – Mtambaswala Km 202.5; Shilingi Bilioni 175.2
Ujenzi unaoendelea
(i) Kidahwe –Kasulu Km 50: Shilingi Bilioni 46
(ii) Nyakanazi – Kakonko Km 50; Shilingi Bilioni 46
(iii)Mafinga –Igawa Km 137.9; Shilingi Bilioni 235.4
(iv)Njombe – Makete Km 107.4; Shilingi Bilioni 217.53
(v)Arusha (Sakina) – Tengeru na mchepuo wa Arusha (Arusha by pass) Km. 56.5; Shilingi Bilioni 145.1
(vi)
Mtwara – Mnivata Km 50; Shilingi Bilioni 89.59. Aidha tunaendelea
kutafuta fedha kutangaza zabuni ya kuunganisha Newala – Masasi.
Wakati
huohuo tunayo miradi iliyo katika maandalizi ya ujenzi na imetengewa
fedha mwaka 2017/2018 yenye urefu wa zaidi ya Km 1,800 kwa thamani ya
Shilingi trilioni 2.99 ikiwemo;
(i) Masasi-Nachingwea – Nanganga Km 91; Shilingi Bilioni 3.5
(ii) Mbinga – Mbambabay Km 67; Shilingi Bilioni 129.3
(iii) Tunduma – Sumbawanga, kazi inaendelea hadi Mpanda – Uvinza (mkandarasi yupo kazini).
Vivuko Na Madaraja
(i)
Tumekamilisha ujenzi wa Kivuko cha juu cha Furahisha – Mwanza kwa
Shilingi Bilioni 7.076 na Daraja la Mto Kilombero kwa Shilingi Bilioni
56.8,
(ii)
Sasa tunajenga madaraja ya juu (Flyover) ya TAZARA kwa Shilingi Bilioni
94, Ubungo Shilingi Bilioni 177.4 na tunatarajia kujenga Kivuko cha
Mwenge.
Tunaimarisha
usafiri jijini Dar-es-Salaam Mabasi Yaendayo Haraka (DART) na tutajenga
awamu tatu nyingine ili kuimarisha usafiri katika Jili la
Dar-es-Salaam kutoka:
§ Katikati ya Jiji – Mbagala
§ Katikati ya Jiji – Gongolamboto
§ Morocco – Mwenge – Tegeta.
Tutajenga pia Bandari Dar-es-Salaam; Bagamoyo; Mtwara.
Serikali
inakusudia kutekeleza miradi iliyopangwa kwenye bajeti zaidi ya km
1,300 na tumefanya upembuzi yakinifu kwa kilometa 1,371. Aidha, Serikali
inaendelea na ukarabati wa barabara za kwenye Miji na Halmashauri
nyingi nchini.
(Kazi za ujenzi wa barabara za lami nchini tumefafanua kwenye Ukurasa 38 – 55)
4.2.2. Usafiri wa Anga
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali
imeimarisha Shirika letu la Ndege ambapo katika mwaka 2016/2017,
Serikali iliingia mkataba wa ununuzi wa ndege mpya sita ambapo ndege
mbili aina ya Bombardier Dash 8 Q 400 ziliwasili nchini Septemba, 2016
na zinaendelea kutoa huduma. Ndege moja, aina ya Bombardier Dash 8 Q 400
imekamilika na itawasili nchini wakati wowote. Ndege mbili aina ya C –
series na Boeing 787-8 Dreamliner 1 zitakuwa zimeingia nchini ifikapo
Juni, 2018.
Serikali
inaendelea na ujenzi wa viwanja vya ndege. Uwanja wa Kimataifa wa JNIA –
ujenzi wa Jengo Jipya (Terminal III) umefikia asilimia 66 na kazi ya
ujenzi inaendelea. Tumekamilisha maeneo ya kusimamia ndege katika uwanja
wetu wa KIA. Tunakamilisha jengo la kupokelea abiria katika Uwanja wa
Ndege wa Songwe. Tumepanua Uwanja wa Ndege wa Dodoma kwa thamani ya
Shilingi Bilioni 60 na tunatarajia kuongeza njia kwa kilometa moja zaidi
ili kuwezesha ndege kubwa zaidi kutua. Tunakamilisha ujenzi wa eneo la
kutua ndege katika Uwanja wa Ndege wa Tabora.
Serikali
imesaini mikataba ya ukarabati na upanuzi wa Viwanja vya Ndege vya
Shinyanga na Sumbawanga. Fedha zimetengwa mwaka huu kwa ajili ya ujenzi
wa Viwanja vya Ndege vya Iringa (Shilingi Bilioni 3.76); Musoma
(Shilingi Bilioni 3.85); Songea (Shilingi Bilioni 3.66); na Mtwara
(Shilingi Bilioni 3.55). Tutatenga fedha kwa ajili ya Viwanja vya Ndege
vya Lindi na Nachingwea. Tunaboresha kwa kuweka taa za kuongozea ndege
na mawasiliano katika Uwanja wa Ndege wa Tabora. Tunarefusha njia ya
kurukia, jengo la kuongozea ndege na jengo la mizigo katika Uwanja wa
Ndege wa Mwanza na kukamilisha jengo la abiria katika Uwanja wa Ndege wa
Kigoma.
4.2.3. Miundombinu ya Reli
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali
imeanza ujenzi wa reli kwa kiwango cha Standard Gauge kutoka
Dar-es-Salaam–Tabora–Kigoma/Mwanza, Tabora–Mpanda, kipande cha Km. 300
kutoka Dar-es-Salaam hadi Morogoro kitakachogharimu Shilingi Trilioni
2.74 umeanza na Mkataba wa kuanza ujenzi wa kipande cha Km. 412 kutoka
Morogoro hadi Dodoma (Makutopora) wenye thamani ya Shilingi Trilioni
4.328 umesainiwa. Aidha, kazi ya upembuzi yakinifu kwa ajili ya ujenzi
wa reli ya Uvinza – Musongati imekamilika.
Serikali
ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali za Rwanda na Burundi
zinaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kugharamia mradi huo. Pia, kazi
ya upembuzi yakinifu na usanifu wa awali wa ujenzi wa reli ya Mtwara –
Songea – Mbamba Bay kwa thamani ya Trilioni 3.99 na matawi ya kwenda
Mchuchuma na Liganga (Km. 1,000) kwa Standard Gauge ilikamilika Juni,
2016. Vilevile, kazi ya usanifu wa kina wa njia ya Reli ya Tanga –
Arusha imekamilika Mei, 2015 na upembuzi yakinifu wa ujenzi wa reli mpya
ya kutoka Arusha hadi Musoma (km 600) na matawi ya Engaruka (km 53),
Minjingu (km 35) na tawi kuelekea Dutwa (km 2.8) pamoja na reli ya
Tabora – Mwanza (km 120) unaendelea.
Tunatarajia kuongeza urefu wa reli kutoka Mpanda hadi Bandari ya Kalemie ili kuhudumia Ziwa Tanganyika.
4.2.4 Usafiri wa Majini
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali
itaimarisha usafiri wa majini kwa kuwa na miradi ya kipaumbele.
Serikali imeanza kutekeleza ahadi ya kuboresha usafiri wa majini kwenye
Ziwa Tanganyika, Nyasa na Victoria.
Ziwa
Tanganyika, taratibu za ununuzi wa Meli mpya unaendelea na watalaam.
Meli ya thamani ya Shilingi Bilioni 24 yenye uwezo wa kubeba abiria 600
na mizigo tani 200 itapatikana.
Ziwa
Victoria, mchakato wa kumpata Mkandari kutoka Korea Kusini umakamilika.
Meli ya thamani ya Dola za Marekani Milioni 37 yenye uwezo wa kubeba
abiria 1,200 na mizigo tani 400 itapatikana.
Kuhusu
Ziwa Nyasa, Serikali imeshapata Meli 2 za mizigo zenye uwezo wa tani
1,000 kila moja kwa thamani ya Shilingi Bilioni 11.252 na sasa
tunakailisha ujenzi wa Meli yenye uwezo wa kubeba abiria 200 na tani 200
za mizigo ya thamani ya Shilingi Bilioni 9.119.
(Mafanikio
tuliyoyapata katika sekta nzima ya Ujenzi na Uchukuzi yameelezwa kwa
kina kuanzia ukurasa wa 41 hadi wa 69 wa vitabu mlivyogawiwa)
4.3. NISHATI
4.3.1. Uzalishaji wa Umeme
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali
inaongeza kiwango cha uzalishaji wa umeme kwa kutekeleza Miradi mikubwa
ya kuzalisha umeme ya Kinyerezi I na II ambayo kwa pamoja inatarajiwa
kuzalisha megawati 565 kwa kutumia gesi asilia kwa gharama ya Shilingi
Trilioni 1.2 na maandalizi kwa ajili ya miradi ya Kinyerezi III na IV
ambayo itazalisha takribani megawati 600 inaendelea. Vilevile, Serikali
imeanza maandalizi ya ujenzi wa mradi mkubwa wa kuzalisha umeme wa maji
wa Staglier’s Gorge ambao utazalisha megawati 2,100. Pia, Serikali
imekamilisha Mradi wa Backbone wa kV 400 unaounganisha mikoa ya Iringa,
Dodoma, Singida na Shinyanga wenye urefu wa Km. 670. Serikali
inashughulikia tatizo kubwa linalokabili Mikoa ya Lindi na Mtwara kukosa
umeme wa uhakika. Tumeagiza mashine zitakazoziba pengo la mashine
zilizoharibika. Pamoja na mashine hizo, Serikali itaunganisha kwenye
gridi ya taifa mikoa hiyo kutoka Dar-es-Salaam.
Serikali
pia inakamilisha ujenzi wa njia ya umeme kutoka Makambako, Njombe,
Madaba, Songea, pia Madaba hadi Ludewa kupitia Liganga. Kazi inaendelea.
Serikali inajenga vituo vya kuongeza nguvu ya umeme Njiro – Arusha,
Mahumbika – Lindi na Madaba – Songea ili kuwezesha usambazaji umeme wa
uhakika hadi vijijini. Aidha, Serikali imeendelea kuhamasisha uzalishaji
wa umeme wa jua kwa kutumia gridi ndogo katika maeneo ambayo hayafikiwi
na Gridi ya Taifa ambapo hadi sasa kuna takribani MW.10 zinazalishwa.
Pia Mradi mkubwa wa Kishapu –Shinyanga MW. 150 unatarajiwa kukamilika
mwaka 2020 na Mradi wa Chuo Kikuu cha Dodoma MW. 55 unatarajiwa
kukamilika mwaka 2019. Kwa sasa mgao umepungua na matarajio yetu ni kuwa
tutauza umeme nje ya Nchi.
4.3.2. Umeme Vijijini
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Kwa
upande wa umeme vijijini, Serikali imekamilisha kwa asilimia 98 Mradi
Kabambe wa Umeme Vijijini Awamu ya Pili (REA Turn-key Projects phase
II), jumla ya wateja 172,000 kati ya wateja 250,000 wameunganishwa na
kazi inaendelea. Wakala wa Kusambaza Nishati Vijijini (REA) imeongezewa
fedha ambapo katika bajeti ya Mwaka 2017/2018, Wakala ilitengewa
Shilingi Bilioni 667.48 ikilinganishwa na Shilingi Bilioni 587.61
zilizotengwa katika Mwaka wa fedha 2016/2017. Duru ya kwanza ya Awamu ya
Tatu ya Mpango Kabambe wa Kusambaza Umeme ambayo imeanza itahusisha
kupatiwa umeme kwa vijiji 3,559 na vijiji vitakavyosalia vinavyofikia
4,314 vitapatiwa umeme katika duru ya pili ya Awamu ya Tatu ikihusisha
maeneo yaliyopo nje ya gridi. Pia, umeme utapelekwa katika maeneo ambayo
hayakupitiwa katika awamu mbili za mwanzo hii ni pamoja na taasisi za
elimu, afya na pampu za maji katika maeneo ya vijijini.
(Mafanikio tuliyoyapata katika Sekta ya Nishati yameelezwa kwa kina kuanzia ukurasa wa 70 hadi wa 74 wa vitabu mlivyogawiwa).
4.4. MAWASILIANO
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu
Serikali
inahakikisha kuwa Taasisi za Elimu, Ofisi za Wakuu wa Wilaya/Polisi,
Hospitali zote za Wilaya, Vyuo Vikuu na Vituo vya Posta 65 ziunganishwe
katika Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano. Kwa kushirikiana na Kampuni ya
VIETTEL hadi kufikia mwezi Septemba, 2017 Serikali imefikisha Mkongo wa
Taifa wa Mawasiliano katika Ofisi za Halmashauri 117, Vituo vya Posta
71, Vituo vya Polisi 129, Hospitali za Wilaya 90, Mahakama 27 na huduma
ya intaneti bure kwa miaka mitatu katika shule 425.
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali
inafikisha huduma za simu za viganjani kwa wananachi wote ambapo
kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Kata 443 zenye uhitaji wa huduma
za mawasiliano zimepata wazabuni wa kupeleka mawasiliano husika. Kati ya
kata hizo 443, upelekaji wa mawasiliano umekamilika katika kata 391 na
Kata 52 zilizobaki zinategemewa kufikishiwa huduma hiyo kabla ya mwisho
wa mwaka 2019. Vilevile, kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Serikali
imetoa zabuni ya kufikisha huduma ya mawasiliano katika kata 75 zenye
vijiji 154 ambazo zinatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Juni, 2018.
Kampuni ya Viattel imepewa zabuni ya kufikisha mawasiliano kwenye vijiji 4,000 vilivyobaki katika mwaka huu wa fedha.
(Mafanikio
tuliyoyapata katika Sekta ya Mawasiliano yameelezwa kwa kina kuanzia
ukurasa wa 74 hadi wa 77 wa vitabu mlivyogawiwa).
5.0. HUDUMA ZA JAMII
5.1. AFYA
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali
inaimarisha huduma za Afya ili ziwafikie wananchi wote hadi vijijini
ili waweze kushiriki katika shughuli mbalimbali za kiuchumi. Katika
kipindi cha kuanzia Novemba, 2015 hadi Novemba 2017, Serikali imeongeza
Vituo vya kutolea huduma za Afya kutoka Vituo 7,014 mwaka 2014/2015 hadi
7,284 mwaka 2016/2017, sawa na ongezeko la Vituo 269. Serikali
imekamilisha ujenzi wa Hospitali za Mlonganzila, Benjamin William Mkapa
na Hospitali za Rufaa kwa ngazi za Mikoa. Wilaya sasa zimeanza kujenga
hospitali na ujenzi umefikia hatua mbalimbali katika maeneo tofauti.
Hivi sasa Halmashauri 15 zinaendelea na ujenzi wa hospitali za Wilaya,
Halmashauri nyingine 15 zipo katika hatua ya kupandisha hadhi Vituo vya
Afya kuwa hospitali za Wilaya na Halmashauri 13 zimetenga maeneo na
kuanza maandalizi ya ujenzi. Hospitali za Mikoa zote sasa zinahamishiwa
Wizara ya Afya.
Aidha,
Serikali imehamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya ambapo
idadi ya watu waliojiunga imeongezeka kufikia asilimia 34 mwaka 2017
kutoka asilimia 19 ya mwaka 2015. Uhamasishaji kwa wananchi walio katika
sekta isiyo rasmi kujiunga na Mfuko wa Afya wa Jamii (CHF) unaendelea
katika Mikoa mbalimbali nchini.
Vilevile,
Serikali imeongeza bajeti ya dawa kutoka Shilingi Bilioni 31 mwaka
2015/16 hadi kufikia Shilingi Bilioni 260 mwaka 2017/2018. Hadi mwezi
Juni, 2017, asilimia 83 ya dawa muhimu zaidi (essential medical items)
zinapatikana katika Bohari ya Dawa na hali ya upatikanaji wa dawa kwenye
Hospitali kufikia mwishoni mwa mwezi Julai 2017 ni asilimia 86.3.
Lengo la Serikali ni kuondoa tatizo la ukosefu wa dawa, Zahanati, Vituo
vya Afya na Hospitali.
(Mafanikio tuliyoyapata katika Sekta ya Afya yameelezwa kwa kina kuanzia ukurasa wa 77 hadi wa 89 wa vitabu mlivyogawiwa).
8.3. ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali
inaboresha Sekta ya Elimu kuwa ya mwelekeo wa Sayansi na Teknolijia ili
kufanikisha ujenzi wa uchumi wa kisasa wa Taifa linalojitegemea.
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali
ya Awamu ya Tano ilianza kutekeleza Mpango wa Elimu Bila Malipo
kuanzia shule za msingi hadi sekondari ambapo tangu Januari, 2016
Serikali ilitenga Shilingi Bilioni 18.77 kila mwezi kwa ajili ya
kugharamia Elimu Bila Malipo. Mwezi Julai 2016, kiasi hicho kiliongezwa
hadi kufikia Shilingi Bilioni 23.868, na hivyo kufanya Serikali kutumia
jumla ya Shilingi Bilioni 465.6 kugharamia elimu bila malipo hadi mwezi
Agosti, 2017. Hatua hiyo imesaidia kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi
walioandikishwa Darasa la I kutoka 1,568,378 mwaka 2015 hadi kufikia
wanafunzi 2,120,667 mwaka 2016. Changamoto iliyojitokeza ni upungufu wa
madawati na Walimu. Madawati yametolewa ya kutosha na ajira za Walimu
zimeanza kutolewa.
Aidha,
Serikali imeweka juhudi katika kujenga maabara ambapo kwa sasa shule za
Serikali zenye maabara ni 2,141 kati ya 3,614 na zisizo za Serikali
zenye maabara ni 1,075 kati ya 1,145. Aidha, Serikali imenunua na
kusambaza vifaa vya maabara vyenye thamani ya Shilingi Bilioni 16.9 kwa
Shule za Sekondari 1,696 kwa ajili ya kuimarisha ufundishaji na
ujifunzaji wa Masomo ya Sayansi kwa nadharia na vitendo.
Vilevile,
Serikali imeongeza Bajeti ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kutoka Shilingi
Bilioni 365 mwka 2015 hadi Shilingi Bilioni 483 mwaka 2017 na kuwezesha
idadi ya Wanafunzi wanaopata Mkopo wa Elimu ya Juu kuongezeka kutoka
98,300 mwaka 2015 hadi wanafunzi 125,000 mwaka 2017.
(Mafanikio tuliyoyapata katika Sekta ya Elimu yameelezwa wa kina kuanzia ukurasa wa 90 hadi wa 100 wa vitabu mlivyogawiwa).
9.4. MAJI
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali imeweka nia ya dhati ya kuwapatia wananchi huduma ya maji safi, salama na ya kutosha, Mheshimiwa Rais ameanzisha kampeni ya kumtua ndoo mama kichwani yenye lengo la kumhudumia mwananchi kupata maji kwa umbali mfupi. Serikali imeboresha huduma ya maji vijijini ambapo hadi Septemba 2017, jumla ya miradi 1,423 ya maji vijijini ilikuwa imekamilika na kufanya jumla ya vituo vya maji vilivyojengwa kwenye miradi kufikia 117,190. Vituo hivyo vina uwezo wa kuhudumia watu 29,297,500, sawa na asilimia 79. Vilevile, Serikali inaendelea kukamilisha miradi mikubwa ya maji ya; kutoa Maji Ziwa Victoria kwenda Miji ya Igunga, Nzega, Sikonge na Tabora kwa thamani ya Shilingi trilioni 1.5, Busega – Bariadi hadi Itirima, Mradi wa Maji Same-Mwanga-Korogwe; Mradi wa Maji wa Chalinze; Mradi wa Maji Kutoka Ziwa Victoria hadi Miji ya Kahama na Shinyanga wa Shilingi trilioni 1.1. Aidha, Serikali inaboresha huduma ya maji katika Miji 17 kwa thamani ya Shilingi trilioni 3.4. Serikali inajenga miradi ya Arusha Jiji – Bilioni 476 na Longido – Bilioni 16. Upanuzi wa mitambo ya kuzalisha maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini, Ulazaji wa bomba kuu kutoka Mlandizi hadi Kimara na ujenzi wa bomba kuu kutoka Ruvu Chini hadi matanki ya Chuo cha Ardhi kwa Jiji la Dar-es-Salaam umekamilka Agosti, 2017. Miradi mingine mingi ipo katika hatua mbalimbali.
(Mafanikio tuliyoyapata katika sekta ya maji yameelezwa kwa kina kuanzia Ukurasa wa 101 hadi wa 111 wa vitabu mlivyogawiwa).
10. KUIMARISHA MUUNGANO
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Katika kipindi hiki vimefanyika vikao vya majadiliano katika ngazi ya Makatibu Wakuu, Mawaziri wa SMT na SMZ chini ya Uongozi wa Makamu wa Rais na kikao cha Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ. Kupitia vikao hivyo baadhi ya changamoto zinaendelea kutafutiwa ufumbuzi. Changamoto hizo ni pamoja na: masuala ya fedha; masuala ya ajira katika taasisi za Muungano na hoja ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia.
Serikali imefuatilia utekelezaji wa miradi na program za pamoja zinazotekelezwa kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
(i) Mpango wa MKURABITA: Mpango huu umeendelea na shughuli za kuandaa, kuongoza na kusimamia utekelezaji wa Mfumo wa Kitaifa wa Umiliki Rasilimali na Uendeshaji Biashara utakaoboresha sheria, kanuni na taratibu za kijamii.
(ii) Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF III): Programu hii imekuwa na mafanikio kwa wananchi wa pande mbili za Muungano ambapo ruzuku zinazotolewa kwa walengwa zimewasaidia kupata mahitaji ya msingi yakiwemo ya chakula, mahitaji ya shule kwa watoto na miradi midogomidogo ya kujiongezea kipato.
(iii) Programu ya Kuendeleza Miundombinu ya Masoko, Uongezaji Thamani ya Mazao na Huduma za Kifedha Vijijini – MIVARF; Programu hii imetekelezwa kwa mafanikio kwa wananchi wa pande mbili za Muungano kwa kujenga miundombinu muhimu ya masoko kuongezewa thamani ya mazao yao, kuwajengea uwezo na kuwaunganisha na masoko na huduma za fedha vijijini.
11. UTAWALA BORA NA DEMOKRASIA
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Mapambano ya dhati ya vitendo vya rushwa, ufisadi na uhujumu uchumi kwa kuanzisha Mahakama Maalumu ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi. Hadi Juni 2017, jumla ya mashauri 30 yalipokelewa ambapo mashauri nane yamesikilizwa kwenye masjala ya Dar-es-Salaam na Mashauri 22 yamesikilizwa katika masjala ndogo zilizopo kwenye kanda mbalimbali za Mahakama Kuu ya Tanzania. Aidha, Serikali imeimarisha mfumo wa utoaji haki kwa kujenga Mahakama za Wilaya na Mahakama ya Mwanzo. Pia, kufanya ufuatiliaji na tathmini ya Usimamizi na Ukaguzi wa shughuli za kimahakama katika mikoa sita ya Dar es Salaam, Pwani, Singida, Tabora, Mwanza na Mara ikihusisha Mahakama za Mwanzo 26, Mahakama za Wilaya 18 na Mahakama za Hakimu Mkazi sita.
12. KUHAMIA MAKAO MAKUU DODOMA
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Tarehe 23 Julai, 2016 ulitangaza uamuzi wa kuhamishia Shughuli za Serikali kutoka Dar-es-Salaam kwenda Dodoma. Awamu ya kwanza ilitekelezwa mwezi Septemba 2016 hadi Novemba 30, 2017 ambapo jumla ya watumishi 2,869 walihamia Dodoma wakiwemo Waziri Mkuu, Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu pamoja na watumishi wengine wa kada mbalimbali. Hivi sasa Serikali inaendelea kuhamisha watumishi Awamu ya Pili na Tatu ambapo watumishi wengine wapatao 5,136 watahamia katika mwaka wa fedha 2017/2018. Aidha, Mheshimiwa Makamu wa Rais amehamia rasmi tarehe 15 Desemba 2017 na Mheshimiwa Rais atahamia wakati wowote hadi 2019.
Katika mwaka wa fedha 2017/2018, Serikali imetenga Shilingi Bilioni 200 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa majengo mapya ya Serikali Dodoma. Ofisi za Umoja wa Mataifa (UN) wameshahamishia Ofisi yao Dodoma.
13. UWEZESHAJI WA WANANCHI KIUCHUMI
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali imehamasisha wananchi kuanzisha na kuendeleza Vyama vya Ushirika katika Mikoa yote ya Tanzania Bara. Hadi kufikia Juni 2017, Vyama vya Ushirika vimeongezeka kufikia 10,596 zikiwemo SACCOs 5,640. Vyama hivyo vina jumla ya wanachama Milioni 1.3 na vina hisa zenye thamani ya Shilingi Bilioni 52.9. Aidha, Serikali kupitia Mifuko mbalimbali imetoa mikopo ya jumla ya Shilingi Trilioni 1.4 kwa zaidi ya wananchi 750,500.
Pia, katika Mwaka 2016/2017, Halmashauri zilitenga Shilingi Bilioni 28.4 kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na Wanawake ambapo hadi Juni, 2017 Shilingi Bilioni 8 zilikopeshwa kwenye vikundi 6,076 vya vijana vyenye wanachama 30,380. Tumeanzisha Mfuko wa Uwezeshaji ndani ya Ofisi ya Waziri Mkuu ambapo pia umeanza kuwezesha makundi ya ushirika vijijini wakiwemo walemavu.
Serikali imeipa SIDO Shilingi Bilioni 7 ili kukopesha wajasiriamali wadogo kwa ajili ya kuanzisha viwanda vidogo. Hata hivyo, Serikali imetoa maelekezo kwa Wakuu wa Wilaya na Mikoa kwa kuwaruhusu Machinga kufanya biashara kwa kuwapangia maeneo mazuri kufanya biashara zao bila bughudha.
14. UJUZI KWA VIJANA
Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa unaelekeza kuweka maeneo mahususi ya kuwezesha vijana wawe na ujuzi stahiki wa kuajirika au kujiajiri katika soko la ajira la ndani na la nje ya Nchi. Katika kutekeleza azma hiyo, Serikali imefanya mambo yafuatayo:-
(i) Kutoa mafunzo ya kukuza ujuzi kwa njia ya uanagenzi (Apprenticeship);
(ii) Kutoa mafunzo ya ujuzi na uzoefu kazini (Internship).
(iii) Kutoa mafunzo ya urasimishaji ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa mafunzo ambayo yanatambua watu wenye ujuzi uliopatikana katika mfumo wa mafunzo usio rasmi.
(iv) Kutoa mafunzo ya kukuza ujuzi kwa walio makazini kwa lengo la kuijengea uwezo nguvukazi iliyopo kazini.
Tangu programu hii ianze kutekelezwa mwaka 2016/17, jumla ya vijana 11,492 wamepatiwa mafunzo katika fani mbalimbali kupitia Vyuo vya umma, binafsi na makampuni. Kati ya vijana hao, 3,000 wamepatiwa mafunzo ya kubuni na kutengeneza nguo kwa kutumia teknolojia za kisasa kupitia viwanda vya Tooku (Dar-es-Salaam) na Mazava (Morogoro). Aidha, zaidi ya vijana 2,600 kati ya waliopata mafunzo hayo wameajiriwa na viwanda hivyo.
15. MWISHO
Serikali yetu inayoongozwa na Rais wetu mpendwa, Dkt. John Pombe Magufuli chini ya Chama cha Mapinduzi bado iko imara.
Nyote mmeshuhudia mengi yaliyofanywa katika kipindi hiki kifupi. TUENDELEE KUMUOMBEA NA KUMUUNGA MKONI. CCM MPYA TANZANIA MPYA.
CCM OYEE!
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!
MAPINDUZI!x2
Ndugu Mwenyekiti naomba kuwasilisha.
Asanteni kwa Kunisikiliza.
(Mafanikio tuliyoyapata katika Sekta ya Elimu yameelezwa wa kina kuanzia ukurasa wa 90 hadi wa 100 wa vitabu mlivyogawiwa).
9.4. MAJI
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali imeweka nia ya dhati ya kuwapatia wananchi huduma ya maji safi, salama na ya kutosha, Mheshimiwa Rais ameanzisha kampeni ya kumtua ndoo mama kichwani yenye lengo la kumhudumia mwananchi kupata maji kwa umbali mfupi. Serikali imeboresha huduma ya maji vijijini ambapo hadi Septemba 2017, jumla ya miradi 1,423 ya maji vijijini ilikuwa imekamilika na kufanya jumla ya vituo vya maji vilivyojengwa kwenye miradi kufikia 117,190. Vituo hivyo vina uwezo wa kuhudumia watu 29,297,500, sawa na asilimia 79. Vilevile, Serikali inaendelea kukamilisha miradi mikubwa ya maji ya; kutoa Maji Ziwa Victoria kwenda Miji ya Igunga, Nzega, Sikonge na Tabora kwa thamani ya Shilingi trilioni 1.5, Busega – Bariadi hadi Itirima, Mradi wa Maji Same-Mwanga-Korogwe; Mradi wa Maji wa Chalinze; Mradi wa Maji Kutoka Ziwa Victoria hadi Miji ya Kahama na Shinyanga wa Shilingi trilioni 1.1. Aidha, Serikali inaboresha huduma ya maji katika Miji 17 kwa thamani ya Shilingi trilioni 3.4. Serikali inajenga miradi ya Arusha Jiji – Bilioni 476 na Longido – Bilioni 16. Upanuzi wa mitambo ya kuzalisha maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini, Ulazaji wa bomba kuu kutoka Mlandizi hadi Kimara na ujenzi wa bomba kuu kutoka Ruvu Chini hadi matanki ya Chuo cha Ardhi kwa Jiji la Dar-es-Salaam umekamilka Agosti, 2017. Miradi mingine mingi ipo katika hatua mbalimbali.
(Mafanikio tuliyoyapata katika sekta ya maji yameelezwa kwa kina kuanzia Ukurasa wa 101 hadi wa 111 wa vitabu mlivyogawiwa).
10. KUIMARISHA MUUNGANO
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Katika kipindi hiki vimefanyika vikao vya majadiliano katika ngazi ya Makatibu Wakuu, Mawaziri wa SMT na SMZ chini ya Uongozi wa Makamu wa Rais na kikao cha Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ. Kupitia vikao hivyo baadhi ya changamoto zinaendelea kutafutiwa ufumbuzi. Changamoto hizo ni pamoja na: masuala ya fedha; masuala ya ajira katika taasisi za Muungano na hoja ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia.
Serikali imefuatilia utekelezaji wa miradi na program za pamoja zinazotekelezwa kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
(i) Mpango wa MKURABITA: Mpango huu umeendelea na shughuli za kuandaa, kuongoza na kusimamia utekelezaji wa Mfumo wa Kitaifa wa Umiliki Rasilimali na Uendeshaji Biashara utakaoboresha sheria, kanuni na taratibu za kijamii.
(ii) Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF III): Programu hii imekuwa na mafanikio kwa wananchi wa pande mbili za Muungano ambapo ruzuku zinazotolewa kwa walengwa zimewasaidia kupata mahitaji ya msingi yakiwemo ya chakula, mahitaji ya shule kwa watoto na miradi midogomidogo ya kujiongezea kipato.
(iii) Programu ya Kuendeleza Miundombinu ya Masoko, Uongezaji Thamani ya Mazao na Huduma za Kifedha Vijijini – MIVARF; Programu hii imetekelezwa kwa mafanikio kwa wananchi wa pande mbili za Muungano kwa kujenga miundombinu muhimu ya masoko kuongezewa thamani ya mazao yao, kuwajengea uwezo na kuwaunganisha na masoko na huduma za fedha vijijini.
11. UTAWALA BORA NA DEMOKRASIA
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Mapambano ya dhati ya vitendo vya rushwa, ufisadi na uhujumu uchumi kwa kuanzisha Mahakama Maalumu ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi. Hadi Juni 2017, jumla ya mashauri 30 yalipokelewa ambapo mashauri nane yamesikilizwa kwenye masjala ya Dar-es-Salaam na Mashauri 22 yamesikilizwa katika masjala ndogo zilizopo kwenye kanda mbalimbali za Mahakama Kuu ya Tanzania. Aidha, Serikali imeimarisha mfumo wa utoaji haki kwa kujenga Mahakama za Wilaya na Mahakama ya Mwanzo. Pia, kufanya ufuatiliaji na tathmini ya Usimamizi na Ukaguzi wa shughuli za kimahakama katika mikoa sita ya Dar es Salaam, Pwani, Singida, Tabora, Mwanza na Mara ikihusisha Mahakama za Mwanzo 26, Mahakama za Wilaya 18 na Mahakama za Hakimu Mkazi sita.
12. KUHAMIA MAKAO MAKUU DODOMA
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Tarehe 23 Julai, 2016 ulitangaza uamuzi wa kuhamishia Shughuli za Serikali kutoka Dar-es-Salaam kwenda Dodoma. Awamu ya kwanza ilitekelezwa mwezi Septemba 2016 hadi Novemba 30, 2017 ambapo jumla ya watumishi 2,869 walihamia Dodoma wakiwemo Waziri Mkuu, Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu pamoja na watumishi wengine wa kada mbalimbali. Hivi sasa Serikali inaendelea kuhamisha watumishi Awamu ya Pili na Tatu ambapo watumishi wengine wapatao 5,136 watahamia katika mwaka wa fedha 2017/2018. Aidha, Mheshimiwa Makamu wa Rais amehamia rasmi tarehe 15 Desemba 2017 na Mheshimiwa Rais atahamia wakati wowote hadi 2019.
Katika mwaka wa fedha 2017/2018, Serikali imetenga Shilingi Bilioni 200 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa majengo mapya ya Serikali Dodoma. Ofisi za Umoja wa Mataifa (UN) wameshahamishia Ofisi yao Dodoma.
13. UWEZESHAJI WA WANANCHI KIUCHUMI
Ndugu Mwenyekiti na WanaCCM wenzangu;
Serikali imehamasisha wananchi kuanzisha na kuendeleza Vyama vya Ushirika katika Mikoa yote ya Tanzania Bara. Hadi kufikia Juni 2017, Vyama vya Ushirika vimeongezeka kufikia 10,596 zikiwemo SACCOs 5,640. Vyama hivyo vina jumla ya wanachama Milioni 1.3 na vina hisa zenye thamani ya Shilingi Bilioni 52.9. Aidha, Serikali kupitia Mifuko mbalimbali imetoa mikopo ya jumla ya Shilingi Trilioni 1.4 kwa zaidi ya wananchi 750,500.
Pia, katika Mwaka 2016/2017, Halmashauri zilitenga Shilingi Bilioni 28.4 kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na Wanawake ambapo hadi Juni, 2017 Shilingi Bilioni 8 zilikopeshwa kwenye vikundi 6,076 vya vijana vyenye wanachama 30,380. Tumeanzisha Mfuko wa Uwezeshaji ndani ya Ofisi ya Waziri Mkuu ambapo pia umeanza kuwezesha makundi ya ushirika vijijini wakiwemo walemavu.
Serikali imeipa SIDO Shilingi Bilioni 7 ili kukopesha wajasiriamali wadogo kwa ajili ya kuanzisha viwanda vidogo. Hata hivyo, Serikali imetoa maelekezo kwa Wakuu wa Wilaya na Mikoa kwa kuwaruhusu Machinga kufanya biashara kwa kuwapangia maeneo mazuri kufanya biashara zao bila bughudha.
14. UJUZI KWA VIJANA
Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa unaelekeza kuweka maeneo mahususi ya kuwezesha vijana wawe na ujuzi stahiki wa kuajirika au kujiajiri katika soko la ajira la ndani na la nje ya Nchi. Katika kutekeleza azma hiyo, Serikali imefanya mambo yafuatayo:-
(i) Kutoa mafunzo ya kukuza ujuzi kwa njia ya uanagenzi (Apprenticeship);
(ii) Kutoa mafunzo ya ujuzi na uzoefu kazini (Internship).
(iii) Kutoa mafunzo ya urasimishaji ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa mafunzo ambayo yanatambua watu wenye ujuzi uliopatikana katika mfumo wa mafunzo usio rasmi.
(iv) Kutoa mafunzo ya kukuza ujuzi kwa walio makazini kwa lengo la kuijengea uwezo nguvukazi iliyopo kazini.
Tangu programu hii ianze kutekelezwa mwaka 2016/17, jumla ya vijana 11,492 wamepatiwa mafunzo katika fani mbalimbali kupitia Vyuo vya umma, binafsi na makampuni. Kati ya vijana hao, 3,000 wamepatiwa mafunzo ya kubuni na kutengeneza nguo kwa kutumia teknolojia za kisasa kupitia viwanda vya Tooku (Dar-es-Salaam) na Mazava (Morogoro). Aidha, zaidi ya vijana 2,600 kati ya waliopata mafunzo hayo wameajiriwa na viwanda hivyo.
15. MWISHO
Serikali yetu inayoongozwa na Rais wetu mpendwa, Dkt. John Pombe Magufuli chini ya Chama cha Mapinduzi bado iko imara.
Nyote mmeshuhudia mengi yaliyofanywa katika kipindi hiki kifupi. TUENDELEE KUMUOMBEA NA KUMUUNGA MKONI. CCM MPYA TANZANIA MPYA.
CCM OYEE!
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!
MAPINDUZI!x2
Ndugu Mwenyekiti naomba kuwasilisha.
Asanteni kwa Kunisikiliza.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )