Mwenyekiti
mpya wa Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli amesema hana
mpango wa kubadilisha Sekretarieti ya chama hicho na itaendelea kama
ilivyo chini ya Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana.
Mwenyekiti huyo mpya alichaguliwa kwenye mkutano wa tisa wa chama hicho uliomalizika jana jioni mjini Dodoma kwa kupata kura zote 1821 za wajumbe wa mkutano mkuu.
Rais Magufuli atahudumu katika nafasi hiyo kwa miaka mitano kuanzia jana hadi mwaka 2022 utakapofanyika uchaguzi mwingine.
Katika
hotuba yake baada ya kuchaguliwa Dkt. Magufuli alisema kwasasa hana
mpango wa kubadilisha Sekretarieti na itaendelea kama ilivyo chini ya
katibu mkuu wa Chama hicho Ndugu Abdulrahman Kinana.
Matokeo
ya Uchaguzi huo yalitangazwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mh. Job Ndugai ambaye aliwataja washindi wote katika nafasi
za Mwenyekiti Taifa, Mwenyekiti Zanzibar na Makamu Mwenyekiti Taifa.
Mbali
na Mwenyekiti wa Taifa lakini pia Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed
Shein alishinda nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Zanzibar kwa kura zote 1821
wakati Ndugu Philip Mangula akishinda nafasi ya Makamu mwenyekiti Taifa
kwa kura zote 1821.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )