Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi
(CCM) , Dkt john pombe Magufuli, amesema kuwa ushindi wa kishindo
uliopatikana katika uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika Novemba 26
mwaka huu umetokana na uimara na ukomavu wa chama hicho.
Rai
Magufuli amesema hayo leo katika Mkutanmo Mkuu Maalum wa Taifa wa CCM
unaoendelea katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Mjini Dodoma na kuongeza
sababu nyingine zilizopelekea kishindo hicho.
Rais
Magufuli ameeleza kuwa ushindi huo unaashiria Matokeo ya kukubalika kwa
Chama cha Mapinduzi pamoja na uimara na ukomavu wa chama hicho.
Ameongeza
kuwa Utekelezaji kwa vitendo mambo waliyoyaahidi wakati wa kampeni za
uchaguzi na Ilani ya uchaguzi ni moja ya sababu zilizopelekea wao
kushinda.
Vilevile
Rais Magufuli ametaja kuwa Umoja na mshikamano mkubwa kati ya wana CCM
umechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza kiwango cha ushindi huo
uliopatikana.
Katika
uchaguzi mdogo wa Madiwani uliofanyika Novemba 26 mwaka huu, Chama cha
Mapinduzi kilipata ushindi wa kata 42 kati ya kata 43 zilizofanya
uchaguzi huku upinzani kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo ukipata
kata moja peke yake.
Aidha
Rais magufuli ameelza kuwa lengo la CCM ni kushinda kwa kishindo zaidi
ambapo wamejipanga kupata ushindi mkubwa zadidi na ikiwezekana wapinzani
wasipate nafasi hata moja.
“Tunataka ikifika uchaguzi mwingine washindani wetu ambao wanatusikiliza humo wasiambulie chochote,” amesema Rais Magufuli.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Abdulrahman Kinana,
yeye ameeleza kuw sababu nyingine zinazopelekea CCM kushinda katika
uchaguzi kuwa pamoja na uwepo wa demokrasia na uhuru wa kujieleza kwa
wanachama wote.
“Watu
wengi wanajiuliza kwanini Chama chetu kinashinda uchaguzi. Sababu kubwa
ya ushindi ni Demokrasia ndani ya Chama. Sababu nyingine kubwa zaidi ni
uhuru wa kujieleza ndani ya chama chetu kila mtu anauwezo wa kusema”
amesema A. Kinana.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )