Mbunge
wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amesema kutupwa ushahidi wao
na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ni kupoteza sifa
na imani kwa wananchi.
Amesema
uamuzi huo unatoa sura ya matabaka kwamba kuna watu ambao wanafikishwa
mbele ya vyombo vya sheria na wengine hawastahili.
Takukuru
kupitia msemaji wake, Musa Misalaba jana Jumapili Desemba 17,2017
alisema taasisi hiyo imeshindwa kuendelea na uchunguzi wa tuhuma za
rushwa zilizowasilishwa na Lema pamoja na mwenzake Joshua Nassari wa
Arumeru Mashariki.
Imesema uamuzi huo unatokana na wabunge hao kuingilia uchunguzi na kuuvuruga licha ya kutahadharishwa kuhusu suala hilo.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Jumatatu Desemba 18,2017 mjini Arusha, Lema
amesema uamuzi wa Takukuru umepoteza imani kwa wananchi ambao walikuwa
na imani na chombo hicho.
Amesema
kitendo cha mamlaka ya uteuzi kumteua waliyemtuhumu, Alexander Mnyeti
kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara kinatoa ujumbe kwa Takukuru.
Akizungumzia hilo, katibu wa Chadema kanda ya kaskazini, Aman Gorugwa amesema Takukuru ilipaswa kutafuta ushahidi.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )