Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri wa Muungano Dkt. John
Pombe Magufuli amefunguka na kutangaza kuuvuruga upinzani Tanzania kwa
kupokea Mbunge mmoja kutoka chama cha upinzani na madiwani wengine saba.
Magufuli
amesema hayo leo kwenye Mkutano Mkuu wa 9 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
ambao umefanyika leo Disemba 18, 2017 mjini Dodoma na kuhudhuriwa na
wajumbe mbalimbali wakiwepo marais wastaafu.
"Nimepokea
majina mengine ya viongozi wa upinzani ambao wanataka kurudi Chama Cha
Mapinduzi (CCM) wasaidizi wangu wameniambia yupo Mbunge mmoja anataka
kurudi na ameniambia kuwa anataka kuja na madiwani saba kwenye jimbo
lake, nasema hiki ni kimbunga na wataisoma namba kweli kweli" alisisitiza Rais Magufuli
Aidha
Magufuli amewataka viongozi wapya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kuhakikisha wanafanya kazi ya kuongeza wanachama wapya katika chama
hicho na kuongeza wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mbali
na hilo Rais Magufuli amesema kuwa wataendelea kupokea na kuwatangaza
watu ambao wanahamia kwenye chama hicho, na kusema kuwa lazima kwanza
wajiridhishe ili wasije kupokea na watu wengine ambao hawana mpango
mzuri kwa CCM.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )