Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli amewatoa
wasiwasi wananchi kwa kusema wazi kwamba anatamani siku moja ifike naye
aitwe mzee mstaafu wa taifa hilo kama alivyo Kikwete na wengine.
Rais
Magufuli ameyasema hayo leo wakati akifungua uchaguzi mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), maarufu kama NEC Taifa, mkoani Dodoma akiwakaribisha
na kuwatambulisha wageni mbalimbali waliohudhuria mkutano huo wakiwemo
Marais wastaafu.
''Natamani siku moja na mimi nistaafu, niitwe mzee mstaafu kama mzee Kikwete niwaachie wengine,'' amesema.
Vipindi
vya ukomo kwa sheria iliyopo kwa nafasi ya Rais ni miaka 10 , sheria
inaruhusu kila baada ya miaka mitano kufanyika kwa uchaguzi mkuu ili
kuwapa demokrasia wananchi kuweza kuchagua kiongozi anayefaa.
Mwezi
Julai, 2017 kuliibuka mijadala mbalimbali katika mitandao ya kijamii
kujadili kauli ya Rais mstaafu ya awamu ya pili Alhaj Ally Hassan
Mwinyi, aliyoitoa katika Baraza la sikukuu ya Iddi aliyosema kama
isingekuwa matakwa ya kikatiba angetegemea kuona Rais aliyepo madarakani
John Pombe Magufuli akipewa nafasi ya kutawala bila kikomo.
Mkutano
huo wa leo utakipatia viongozi wapya wa ngazi ya juu chama hicho
ikiwemo Mwenyekiti taifa na Mwenyekiti baraza la mapinduzi Zanzibar.
Tayari Rais magufuli amethibitisha kuwa katibu mkuu wa chama hicho Abdulrahman Kinana ataendelea na nafasi yake.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )