Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU imekanusha taarifa
zilizosambaa mtandaoni kuwa wanamshikilia aliyekuwa Mkurugenzi wa
Shirika la Nyumba la Taifa NHC Nehemia Mchechu.
Afisa
habari wa TAKUKURU Musa Misalaba amesema wanashangaa taarifa hizo
zimetoka wapi na wao kama taasisi hawamshikilii Mkurugenzi huyo
aliyesimamishwa na Waziri Lukuvi wiki iliyopita.
“Hizo
taarifa sijui zimetoka wapi, lakini sisi hatuna huyo mtu, hatujamkamata
saa tunashindwa kuelewa watu wanazusha kwa lengo gani”, amesema
Misalaba.
Aidha
msemaji huyo ameongeza kuwa wao kama taasisi hawajapokea agizo lolote
la kumkamata na kumfanyia uchunguzi ndugu Nehemia Mchechu hivyo hawana
sababu ya kumkamata.
Nehemia
alisimamishwa kazi na Waziiri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mh. William Lukuvi siku ya Jumamosi wiki iliyopita. Jana jioni kwenye
mitandao zilisambaa taarifa za kukamatwa kwake ambavyo leo TAKUKURU
imekanusha.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )