Katibu
mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana leo ameteuliwa
na Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais John Pombe Magufuli kuendelea kuwa
katika nafasi yake kwa kipindi kingine.
Akiongea
katika mkutano wa 9 wa Chama hicho unaoendelea mkoani Dodoma
amemshukuru kwa kazi yake nzuri kwa muda wote ambao amekuwa katika
nafasi hiyo huku akiweka wazi kuwa ni lazima aendelee kufanya nay kazi
kwasababu ameridhishwa na utendaji wake wa kazi.
''Namshukuru
ndugu Kinana kwa msaada wake mkubwa alionipa kwa kipindi chote hicho
nafikiri anafaa kuendelea kuwa katika nafasi hiyo kwa kipindi
kingine,'' amesema Magufuli.
Kauli
ya Rais Magufuli inaondoa tetesi zote zilizokuwa zinadai kuwa Kinana
ameandika barua ya kuomba kujiudhuru katika nafasi yake kwa kilichodaiwa
kuwa haridhishwi na utendaji wa Mwenyekiti wake Rais Magufuli.
Baada
ya kupata nafasi hiyo Abdulrahman Kinana amemshukuru Rais Magufuli kwa
kumuamini pamoja na kuahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili
kukijenga chama hicho pamoja na nchi kwa ujumla.
Kinana
aliwahi kuwa mtumishi wa Jeshi la Tanzania kwa miaka 20 pamoja na kuwa
Spika wa kwanza wa Bunge la Afrika Mashariki mwaka 2001 hadi 2006,
amechaguliwa kuwa Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), tangu 2012.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )