Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
MAKAMU
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan
amekataa kuzindua stendi kuu mpya ya Mailmoja Kibaha mkoani Pwani, akiwa
katika ziara yake mkoani humo.
Hatua
hiyo ameifikia kutokana na kupata wasiwasi wa utekelezaji wa mradi kuwa
na baadhi ya mapungufu ambapo amedai baada ya kufanya uchunguzi wiki
mbili ama tatu zijazo atakwenda kuuzindua.
Akizungumza
katika stand hiyo, Samia alieleza, kuna minong’ono wameisikia kuhusu
mradi huo hivyo ni jukumu lake kuibeba na atakapo jiridhisha atarudi kwa
mara nyingine .
Hata hivyo, alisema atakutana na mkuu wa wilaya, mkurugenzi na mkuu wa mkoa kuzungumzia suala hilo.
“Msishtuke
kwa hili ni kawaida kwa kuchukua hatua za aina hii ili kujiridhisha kwa
maslahi ya halmashauri, mkoa na watumiaji kijumla “
“Serikali
ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni sikivu na kusikia malalamiko ya
wananchi, tumepata malalamiko kidogo kuhusu stand hii, serikali ni ya
uwazi na ukweli hivyo sitofungua stendi “alisisitiza Samia.
Samia
alimpongeza mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kibaha, Jennifer Omolo
na mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama na wahusika waliohusika
kufanikisha mradi huo.
Nae
waziri wa nchi ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa
-TAMISEMI ,Selemani Jafo alisema yeye kama waziri wapo wataalamu
wanaohakiki lakini ameridhishwa na kazi hiyo .
“Kwani kila kazi ina changamoto za kibinadamu, hasi na chanya, lakini wamejitahidi “alisema Jafo.
Jafo
alieleza, mradi huo umepata msaada wa mkopo nafuu kutoka bank ya Dunia
ambao wamepata fedha za kimarekani dollar milioni 255 .
Alielezea
, wanagusa miji 18 na wanachokifanya wanagusa stendi tisa, barabara za
miji kwa kiwango cha lami na madaraja makubwa ya kisasa.
Wakitoa
kero ya stand hiyo, madereva pikipiki walidai eneo lililotengwa kwa
ajili yao halina sehemu ya kujikinga hivyo kusababisha usumbufu wakati
wa mvua na jua.
Mkurugenzi
wa halmashauri ya mji wa Kibaha, Jennifer Omolo alisema katika stendi
ndogo ya awali walikuwa wakikusanya ushuru sh. 950.000 kwa siku ambapo
sasa wanakusanya sh. milioni 1.6 .
Alisema
mradi huo umegharimu sh. bilioni 2.9 na walishamlipa mkandarasi bilioni
2.7 ,stendi hiyo itakuwa na mabanda kumi ya kukatia tiketi, mawakala 40
,eneo la tax, na wafanyabiashara ndogondogo wanaojiingizia kipato kwa
kuuza biashara zao wapo 100 .
Samia
akiwa katika ziara yake Kibaha vijijini na mjini pia alipata fursa ya
kutembelea mradi wa reli ya kisasa ya standard gauge kujionea namna
unavyoendelea.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )