Wananchi wa
familia saba za kijiji cha Sakila kilichopo kata ya kikatiti wilayani
Arumeru mkoani Arusha wanalala nje na watoto wao huku wakikabiliwa na
njaa kali baada ya watu wanaodai kutumwa na serikali ya kijiji kuvunja
nyumba zao na kufyeka migomba yao.
Wakizungumza na
ITV wananchi hao wanaodai kuwa wameishi maeneo hayo kwa zaidi ya miaka
30 wamesema wanashangazwa na viongozi wa kijiji hicho kutoa baraka za
kuvunja kwa nyumba zao kwa kisingizio kwamba wao ni wavamizi.
Mwenyekiti wa
kijiji hicho Bw Richard Mbise amesema hatua hiyo imekuja baada ya
mahakama kuthibitisha kuwa wananchi hao walivamia eneo hilo na walikiuka
taratibu.
Hata hivyo
baadhi ya viongozi wastaafu wa vijiji vya kata hiyo pamoja na kukiri
kuwepo kwa mgogoro huo wamesema hatua ya zinazochukuliwa kuutatua
zikiwemo za kuvuja nyumba na kukata migomba sio sahihi.
Tatizo la
migogoro ya ardhi katika wilaya ya Arumeru ambalo kwa sasa linaelekea
kuwa sugu limeendelea kuwaathiri wananchi wa huku baadhi ya viongozi
wakiwemo wa kisiasa wakilitumia kama ajenda za kutafuta maslahi yao
jambo ambalo lisipodhibitiwa linaweza kuleta maafa makubwa.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )