Unakumbuka
Video ya Nitarejea ya Diamond? Basi yule msichana aliyeshirikiana naye
katika huo wimbo hali yake si nzuri kisanii na kimaslahi pia kiasa cha
kusema kuwa anauchukia huo wimbo kwani ndo umemuharibia Maisha
Hawa
akihojiwa na Mlimani TV amefunguka na kusema kuwa Pamoja na Wimbo huo
kuwa ndio uliomtoa Diamond Kimuziki lakini Diamond hakuwahi kumpa Hata
Shiling 10 , Japo ameshawahi kumfuata na kumuomba msaada wakati tofauti
tofauti lakini haikuwezekana kupata huo msaada ....Hawa amesema
alitegemea nae angetoka lakini ameishia kuwa na maisha ya Dhiki huku
mwenzake akitengeneza Hela za Maana ..
Alipoulizwa
Kuhusu tuhuma za kutumia Madawa ya Kulevya baada ya kuona mambo
hayaendi vizuri Hawa amesema hakuwahi kutumia Madawa ya Kulevya bali
alijiingiza katika unywaji wa pombe sana baada ya Mwanaume aliyempa
Mimba Kumkimbia hivyo alianza matumizi ya pombe kupunguza Mawazo ..
Hawa anasema Hamchukii Diamond ila Anapenda kumwambia akumbuke alipotoka na Arejee Nyumbani...
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )