Featured
Loading...

MRISHO MPOTO AIBIWA VITU VYA NDANI VYENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 7 Mpoto



Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto amejikuta mpweke baada ya kupuliziwa dawa na wezi na kuibiwa vitu vya ndani vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 7 usiku wa kuamkia leo.


Akizungumza kwa masikitiko, Mpoto amesema wezi hao huenda waliwapulizia dawa hali ambayo ilisababisha kutoshtukia mchezo huo.
11137939_1417735698533088_783799092_n
Sehemu ya TV na radio


“Yaani wamesafisha kila kitu,” amesema Mpoto. “Hapa sebuleni hakuna kitu yaani. Mimi mwenyewe nilikuwepo sema labda ni kwa sababu nyumba kubwa pia tunahisi labda walitumia dawa kwa sababu sio kawada nikalala hivyo bila kusikia kinachoendelea. Nahisi walitupulizia dawa za usingizi. Pesa nyingi sana ni zaidi ya milioni 7, sema tayari suala nimelifikisha polisi na wanaendelea na upelelezi. Wameiba vitu ni vingi, flati screen, maredio yaani ni vingi.”
Mpoto

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top