Wazo hili limezaliwa ndani ya ule mfumo huru wa safari za ndani ya bara la Ulaya ambapo nchi zake zote hufanya safari bila visa ndani ya bara hilo. Mpaka sasa nchi 13 za Afrika zina mikataba ya safari za bila visa kwa nchi nyingine za ndani ya Afrika, ambapo raia wake usafiri bila ya visa ama kupokea visa wanapowasili.
Viongozi wa nchi za Afrika watakapokutana Kigali Rwanda July 2016 watakuwa miongoni mwa watu wa kwanza kutumia passport hizo za kielektroniki. Lengo ni kurahisisha safari za ndani ya Afrika
na inaaminika pia biashara za ndani zitaimarika na kukuza uchumi kwa
ujumla pia kuimarisha ujamaa na mahusiano mazuri baina ya nchi hizo.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )