Mwanadamu ameumbwa na kiu kubwa ya kupenda kuwa sahihi, kuonekana anaweza na pia kujiona kuwa anafaa na kukubalika. Kutokana na ukweli huo Mwanadamu anajiona kuwa anao wajibu wa kufanikiwa na kukubalika kutokana na mafanikio ayapatayo katika maeneo mbalimbali katika maisha yake. Hatari iliopo kwa kila mwanadamu ni pale anapojikuta ameshindwa kufanikiwa na ili asijilaumu yeye mwenyeawe anamsingizia mtu mwingine au mazingira aliyopo. Mwanadamu wa kwanza kushindwa kutii amri aliyopewa na Mungu nakula tunda walilokatazwa alitoa kusingizio kwa kushindwa kutii amri aliyopewa hebu msikilize hapa,“ Adamu akasema, Huyo Mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala Bwana Mungu akamwambia mwanamke Ni nini ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya nikala” Pamoja na visingizio walivyotoa wazazi wetu wa kwanza adhabu walipewa na Mungu mwenye haki. Kwa maneno mengine ni kwamba ukosefu wa umakini au uangalifu lazima utatuletea majanga ya aina fulani kwani ni wajibu wetu kujitahidi kuepuka makosa au kushughulikia madhaifu tuyaonayo katika mahusiano yetu.
Kuna sababu
mabalimbalil zinazopelekea mtu kutoa visingizio lakini wengi hutoa visingizio
kwa sababu zifuatazo.
1. Kuogopa kufikiriwa vibaya
2. Kuogopa kushindwa
3. Kuogopa mabadiliko
4. Kuogopa kuwajibika
5. Kuogopa kufanya kosa
6. Kuogopa ugomvi
7. Kuogopa kuonekana hujui au huwezi.
Watu wanaotumia
visingizio mbalimbali kuhalalisha matatizo au madhaifu yao hawajui kuwa
wanajikosesha fursa ya kujifunza mambo mapya na kutatua matatizo yao na hivyo
kutengeneza mazingira mazuri ya kimapenzi.
Vifuatavyo ni
visingizio mbalimbali ambavyo wapendanao hutumia kuharibu ubora wa husiano wao.
1. SINA MUDA WA KUTOSHA
Mwanzoni mwa
mahusiano ya kimapenzi utaona wazi kuwa mpenzi wako anafanya jitihada kubwa za
kutafuta muda wa kuwa na wewe au kuongea na wewe kwenye simu lakini baada ya muda
fulani unasikia mpenzi yule yule anasema kuwa ana kazi nyingi ( yuko bize) na
hana muda wa kuwa na wewe au kuongea na wewe.Hivi karibuni nimesikia kisa cha
dada ambae mpenzi wake aliemzoesha kumpigia mara kwa mara na baadae
kuacha kufanya hivyo, kaka huyo alitoa kisingizio cha kukusa salio la
muda wa hewani na dada huyo alipofuatilia aliona ni ukweli kwani biashara ya
kaka huyo ilikuwa na hali mbaya.Nilifurahi kusikia kisingizio hicho toka kwa
mwanaume kwani kwa sehemu kubwa wanawake wengi ni sugu katika kutumia
kisingiizio hicho .Swala la mtu kutumia kisingizio cha ubize mara kwa mara ni
dalili ya penzi kunyauka. Uonapo hilo limeanza kujitokeza tambua kwa hakika
kuwa penzi lake kwako limeanza kubadili muelekeo na huko
linakoelekea ndiko alikokazia macho yake na sio rahisi kukukumbuka
wewe. Iwapo utaamini hilo na mtu huyo bado anadai yupo bize nab ado anakupenda
basi tambua unayokazi ya kuleta mabadiliko ili mrudie hali ya mwanzoni. Hebu
fikiria yafuatayo kwa mtu anaesema yuko bize, Iwapo tuko bize sana tukashindwa
hata kupika chakula – tutakufa njaa. Iwapo tuko bize sana tukashindwa kufanya
usafi wa miili na nyumba zetu tutanuka na kupata magonjwa. Kwa maneno mengine
mpenzi wako naposema yupo bize mara kwa mara maana yake ni kwamba haoni
uthamani wa uhusiano wenu na hajali iwapo utaharibika kwa ukosefu wa muda wa
kujenga na kuimarisha uhusiano wenu.
Hebu fikiria mfano
mwingine, mtu anasema “ napenda sana kujisomea BIBLIA au Quran lakini nakosa
muda wa kujisomea” Je mtu huyo huyo iwapo anatumia muda mrefu kuangalia TV au
Kuchat na marafiki zake kweli utasema kweli anapenda kusoma BiBlia au Quran?
Kila mmoja wetu
ana masaa 168 kila wiki na iwapo unatoa kipaumbele kwa mpenzi wako lazima uamue
kupunguza mambo mengi ila ufanya mambo ambayo yatamthibitisha mpenzi wako kuwa
ni wa muhimu kwako.KWA mtu anaekupenda lazima atoe kipaumbele kwako kwa kuweka
mabo mengine pembeni.Kuelewa vizuri maneeno yangu fikiria juu ya mzazi kuacha
starehe ya pombe ili fedha zitumike katika kusomesha mtoto wake,au pale unapomnunulia
mpenzi wako zawadi haimaniishi kuwa fedha unazotumia hazina kazi kwa upande
wako bali unataka umfurahishe mpenzi wako.
2. VISINGIZIO VYA KUTOJUA
Watu wengi wamekuta
mahusiano yao yanaharibika kwa kuwa hawakufanya bidii kufahamu mambo mengi juu
ya wapenzi wao na hivyo kusubiri kuambiwa kila kitu. Unaposubiri uambiwe kila
jambo unamboa mpenzi wako. Nakumbuka siku moja kupokea sms toka kwa mpenzi
wangu na ilikuwa jioni ambapo nilikuwa nimechoka na sikupenda kujibu kwa
sms. Nilimpigia mpenzi wangu na simu haikupokelewa na ukapita muda
hakunipigia, baadae kidogo kanibip, nikachelewa kumpigia kwa kuwa nilikuawa
naongea na simu nyingine, nilipomaliza nikampigia kwa mara ya pili tena simu
haikupokelewa. Baadae nilipoonyesha kuwa nimekasikirika kwa yeye kushindwa
kupokea simu yangu akasema kuwa “ Yeye alijua kuwa meseji yake ningeijibu kwa
meseji na hakujua kuwa ningepiga badala yake. Niliumia na kumuuliza, “Je,
tumewekeana mkataba kuwa sms lazima ijibiwe na sms” akasema, hapana .Ndugu
yangu unaona kisingizio alichotumia mpenzi huyo? Anasema alikuwa hajui kuwa upo
uwezekana wa mimi kupiga baada ya kukuta sms yake. Je kisingizio hicho
kitasaidia kujenga penzi au kubomoa?
Kuna watu wengi wanaleta
utani unaofanana na ukweli na mpenzi anapokasirika kutokana na utani huo
hujitetea kuwa “ nilikuwa sijui kuwa itakuumiza hivyo” Mtu mmoja ambae alikuwa
anachukia watu wanaotumia visingizio alisema hivi. Mimi huvunja uhusiano haraka
sana. Sitaki nizeeke kwa kumwelezea mtu mzima wapi ananiboa” Mtu huyo
anaonyesha ni jinsi gani uzembe wa aina yoyote ni kosa la jinai kwake.Ni muhimu
ndugu yangu ujitahidi kuwa makini kwani haiwezekani kuwa mpenzi wako atakuambia
kila kitu anachohitaji au kukichukia, ni juu yako kuonyesha penzi la kweli kwa
kujitahidi kuongezea maarifa ili uwe bingwa katika kila eneo la uhusiano
wako.Itakuwa rahisi kwa penzi kati yenu kuongezeka iwapo mtajenga mazingira ya
uwazi a,\mbapo unajisikia huru kuuliza maswali mbalimbali.
3. VISINGIZIO VYA KIFEDHA
Kwa sehemu kubwa
mahusiano ya kimapenzi huhusisha fedha katika maeneo mbalimbali, muda wa
maongezi kwa njia ya simu, gharama ya vyakula na vinywaji, zawadi za hapo na
pale na mahitaji mengine muhimu. Tafiti zinawaonyesha kuwa pale mpenzi mmoja
aonapo mwenziwe anatumia fedha vibaya kiwango cha penzi na furaha kati yao
hupungua. Hebu fikiria ukweli wa utafiti huo, Je sio kweli kuwa mke ambae
anamwona mume wake kuwa hawezi kulala bila kunywa pombe ataongezeka furaha au
furaha itapungua, Je mume anaemuona mke wake anapenda kununua nguo za bei mbaya
kila mwisho wa mwezi je furaha yake itaongezeka au itapungua? Ni muhimu uone
kuwa kupungua kwa furaha kwa mmoja kutaathiri uwezo wake wa kuonyesha
penzi motomoto na
hivyo kuweka uhusiano wenu katika eneo la hatari. Eneo lingine la kifedha
ambalo ni hatarishi ni kuficha matumizi makubwa au matumizi yasiokubalika. Mtu
atapewa Ths. 50,000/= kwa ajili ya mahitaji muhimu anatumia Tsh. 40,000/= na
nyingine anatumia kwa matumizi yake binafsi. Anasema sina hela kumbe anazo na
anaziweka kwa ajili ya matumizi haramu. Watu wengi hutumia visingizio
mbalimbali kuhalalisha kutotumia fedha zao kwa ajili ya wawapendanao au
kujifanya hana fedha ili kumnyonya mwingine. Visingizio hivyo unaweza kuvitumia
na kujiona mjanja kumbe mwenzio anajua unamdanganya na visingizio vyote
utumiavyo ni uongo mtupu. Kwa kuwa mpenzi wako hataweza kukuambia juu ya hisia
zake juu ya matumizi yako ya fedha au utegemezi wako wa fedha kwake ,taratibu
penzi kati yenu linanyauka hadi kufa Kabisa.
VISINGIZIO VYA
KURUHUSU MAOVU DHIDI YAKO YAENDELEE.
Sikatai kwamba ni
kweli mara nyingine mpenzi wako kweli kabisa anakuwa na kazi nyingi kuliko
kawaida lakini kamwe usianze kumtetea ili kuhalalisha visingizio vyake
iwapo unaona wazi kuwa iwapo angefanya bidii lazima angepata muda wa
kukuonyesha wewe kuwa ni mtu wa muhimu katika maisha yake. Mtu anakwambia yuko
bize kweli kama kweli anakupenda hawezi kuamka saa 8 za usiku na kukutafuta,
ndio anatumia kisingizio kuwa amechoka na kazi na hamuwezi kucheza ngoma
ya wakubwa je kweli haweza kujitolea akakuamsha saa 9 usiku mkacheza ngoma
hiyo? Ukishindwa kumkabili na kumwonyesha ulemavu wa kisingizio chake utaendelea
kujidanya kuwa unapendwa kumbe mwenzi ameshakuwa msagaji au shoga. Tambua kuwa
nyuma ya kila kisingizio kunasababu usioambiwa ya yeye kusema hivyo. Usiruhusu
mpenzi wako aamini kuwa utakubaliana na kisingizio chochote anachotoa.
Iwapo unajikuta
unakubaliana kwa urahisi na visingizio vya mpenzi wako tambua kuwa uko katika
uhusiano ambayo kamwe hutaweza kuwa na furaha ya kudumu. Ni kweli kabisa kuwa
unampenda sana mpenzi wako anaekuumiza lakini ni muhimu ukumbuke kuwa
hustahili kuwa mtu wa kuumizwa umizwa mara kwa mara haswa na mtu anaendai kuwa
anakupenda. Sio hilo tu na hata pale ambapo unajikuta una mpenzi anaeboa mara
kwa mara na moyoni unaona kuwa kwa uhusiano wa muda mrefu mtu huyu hafai ,ni
vyema kusikiliza moyo wako badala ya kutafuta visingizio vya wewe kuendelea na
uhusiano usiiokusisimua kama unavyotamani iwe. Ni kweli hajakufanyia uhalifu
mkubwa lakini iwapo haonyeshi bidii ya kuleta uchangamfu na raha unayohitaji ni
wakati wa kufikiria upya juu ya uhusiano huo. Bila shaka umeshawahi kusikia mtu
akisema, “Akiwepo fulani nyumba inachangamka sana.” Maneno hayo ni ushahidi
kuwa uchangamfu ni wa muhimu sana miongoni mwa wapendanao.
Ndugu yangu, ni wakati wa kupiga vita visingizio vyoyote anavyotumia mpenzi wako kukukosesha raha na wewe mwenyewe upigi vita visingizio vinavyomkosesha raha mpenzi wako.Katika utafiti uliofanyika huko UINGEREZA na shirika la sheria liitwalo Slater and Gordon UNAONYESHA KUWA watu wengi hubakia kwenye mahusiano yanayowaumiza kwa visingizio vya aibu ya kuachwa,woga wa kubakia bila mpenzi au woga wa kukosa fedha walizokuwa wanapata kwa mpenzi huyo mtesaji.Ni wakati sasa wa kuangalia upya kiwango cha furaha kati yenu kama kinaridhisha, kama hakiridhishi angalia nia aina gani ya visingizio vinatumika kuendeleza maumivu kati yenu na kupambana na visingizio hivyo kikamilifu.
PENZI LINAPOGEKA KUWA
KERO
Mahusiano ya kimapenzi ni kitu kizuri
sana ndio maana mara ya kwanza mtu anapoingia katika mahusiano ya kimapenzi
anakuwa na furaha kubwa sana. Naomba uzingatie kuwa nimesema kuwa mtu
anapoingia katika uhusiano kwa mara ya kwanza, yaani kama ni
mwanaume huyo anakuwa ndie mwanamke wa kwanza kabisa kwake
na kwa mwanamke huyo ndio anakuwa mwanaume
wa kwanza kabisa. Katika ulimwengu tulionao sasa ni mara chache sana
utaona kuwa mwanaume ambaye hajawahi kuwa na mahusiano ya kimahaba NA
MWANAMKE anaanza na mwanamke ambaye na yeye huyo ndio anaekuwa mwanaume wa
kwanza.
Tatizo tulilonalo sasa utakuta mwanaume
ambaye tayari ameshakuwa na mahusiano na wanawake 2 anaanza uhusiano na dada
ambaye hajakuwa na uhusiano wowote au dada ambaye ameshakuwa na mahusiano na
wanaume wawili anaanza mahusiano na mwanaume ambae hajawa katika mahusiano ya
kimapenzi.Katika mazingira kama hayo lazima mtu atajikuta analinganisha mpenzi
aliene sasa na Yule aliemtangulia.
Katika kazi yangu katika Clinic ya afya
ya mapenzi huu ni mwaka wa kumi toka nianze vipindi redioni na mara chache
katika TV na asilimia zaidi ya 95% ya wateja wanaofika ofisini kwangu ni
wanaume na asilimia kati ya 30 hadi 40ni wanawake .Asilimia kubwa ya wanaume
wanaokuja ofisini kwangu wana matatizo ya nguvu za kiume au kuwahi kumaliza
upandaji wa mbegu dume.
Vilio vingi toka kwa wanawake ni
kutoridhika na raha wanayoipata katika uchezaji wa ngoma ya wakubwa na ukosefu
wa penzi wanalohitaji na hasa kushuka kwa mawasiliano na muda wa kuka
pamoja. Wakati wanaume wanalalamika kuwa wanawake wanawanyima haki zao za
kucheza ngoma ya wakubwa wanawake wanalalamika kuwa hawafurahii kucheza ngoma
ya wakubwa na wapenzi wao.BILA shaka hapo unaweza kuona chimbuko l mvutano
unaotokea katika mahusiano mengi ya kimapenzi.
Tafiti baada ya tafiti zinathibitisha
kuwa udhaifu au uzembe katika kucheza ngoma ya wakubwa unachangia sana katika
migogoro inayojitokeza katika mahusiano ya kimapenzi na zifuatazo ni SMS toka
kwa wasikilizaji wangu wa redio, SMS, ambazo zinaonyesha jinsi gani penzi
linaweza kugeuka kuwa kero kubwa
‘Dr. Nelson mimi ni kijana
wa umri wa miaka 25 nimekuwa na mahusiano na dada mmoja na huu tunaingia
mwezi wa 3 cha ajabu ni kwamba dada huyo hakuwahi kuniambia kuwa ameolewe
na nikajikuta nampenda sana huyo dada.
Sasa nimegundua kuwa ni mke wa
mtu na nashindwa kumuacha japo na mimi nina mchumba. Sasa Dr. huyo mke wa
mtu anataka azae na mimi jambo ambalo linanichanganya akili na kuniletea
kishawishi cha kufanya jitihada nivunje ndoa yake nimuoe yeye Dr. nifanyeje?.”
“Dr. Nelson mimi naitwa Issa nina umri
wa miaka 29 nimeoa toka mwaka juzi. Tatizo ni kwamba kila nikimwambia mke
wangu kitu cha maana kama hajakipenda huniambia nitaenda kuolewa na mwanaume
mwingine kwani mwanaume sio wewe peke yako, mbaya zaidi wakati wa kucheza ngoma
ya wakubwa yaani hata kabla sijamaliza ananiambia toka mimi nimechoka na mimi
kulazimika kumaliza haraka haraka. Dr. hali hiyo inanichukiza sana naomba
unisaidie hali hiyo inasababishwa na nini?.”
“Kwa jina naitwa Joyce niliishi vizuri
na mume wangu ikafika sehemu akaona simtoshelezi na akanisaliti na kuniambukiza
magonywa ya zinaa mara 2. Hayo yakanifanya niende nje ya ndoa ili nipata kujua
nina utamu au uchungu, nikashangaa napewa sifa kibao n huduma kupewa
nikaanza kumnyima mume wangu unyumba na kuacha aendelee na dogo dogo.”
“Dr. mimi niko kwenye ndoa mwaka wa 11
mke wangu hunipa unyumba kwa shingo upande. Pia ameshanitamkia kuwa hanipendi
mimi nampenda Dr. nifanyeje ili upendo urudi?.”
“Dr. Nelson asante sana kwa mafundisho
yako ambayo yanatupa tumaini kuwa upo uwezekano wa mtu kufurahia ndoa siku
zote. Niko ndani ya ndoa na nina tatizo. Toka niolewe na mume wangu
ninapomsemesha anakuwa mkali na akiwa nyumbani ni kimya hamna mazungumzo na
mara nyingine yuko bize na simu. Siku akikusemesha vizuri ujue anataka umpe
ngoma ya wakubwa acheze unanishaurije hapo?.”
Kesi ya kwanza ni ya mwana mke
aliechepuka kwa kijana ambae hajaoa na akajikuta amekolea penzi mpaka anataka
atengeneze kumbukumbu ya utamu aliopata kwa kuzaa na mwanaume mwingine na
kesi ya pili ni ya mwanamke ambae hampendi mume wake na si ajabu ana
mchepuko. Je ni mambo gani ambayo yanachangia katika kuleta mikorogano
mbalimbali miongoni mwa wapendanao? Najua yapo mambo mengi sana kama matatizo
ya kifedha, uchafu, wivu, ndugu, unene na ukosefu wa uwazi na maongezi ya
kutosha baina ya wapendano pamoja na madhaifu katika utendaji wa tendo la ndoa.
Lakini kwa kuwa sayansi ya mapenzi inathibitisha kwa kati ya asilimia 80% hadi
85% ya migogoro yote katika ndoa chimbuko lake ni hitilafu katika kucheza ngoma
ya wakubwa upo umuhimu wa kuangalia eneo hilo kwa makini sana.
Ni vyema tuangalie eneo hilo kwa upya
na kwa umakini mkubwa sana. Mwanzoni mwa uhusiano kwa wengi kila kitu ni
kipya na chenye uwezo mkubwa wa kuleta msisimko mkubwa na mmoja au wote
hupenda hali hiyo tamu iendelee milele. Lakini kwa bahati mbaya mwanamke
atapata shida kufika kileleni iwapo atakuwa katika mazingira ambayo yanamletea
huzuni, wasiwasi, kutojiamini, hasira au kuwa na hali ya kujiona kama mtu
alieshindwa.
Mwanamke atajiona kama mtu alieshindwa
pale anapojiona kuwa ni mnene na hataki unene, pale anapojiona kuwa hana fedha
za kufanya hili na lile kama marafiki au majirani wanavyoweza kufanya na mbaya
zaidi akiwa na mume ambaye hawi karibu na yeye mara kwa mara inatengeneza
uchungu nafsini mwake.
Mwanaume anaposhindwa kuwa karibu na
mpenzi wake mara kwa mara mwanamke hujisikia vibaya kwa kuwa anajiona kama hana
mvuto mkubwa sawa na yule mama aliechepuka, na huko kwenye mchepuko akajikuta
anasifiwa na kuonyeshwa kuwa ni mtu wa muhimu kwa mafunzo aliopata mchepukoni.
Kama ulivyoona kwenye stori hiyo mama
huyo baada yakupata mchepuko aliona uhalali wa kumnyima unyumba mume wake na
moyo wake usimhukumu kabisa.
DR. David Barlow wa chuo kikuu cha
Boston huko Marekani katika utafiti wake wa kina ameshuhudia kuwa mwanamke
ambaye huko nyuma ameshawahi kuwa na mwanaume mwenye matatizo ya nguvu za kiume
au kuwahi kumaliza au kukosa hamu ya tendo la ndoa, anapojikuta mume aliyenae
sasa ameanza kuonyesha madhaifu kama hayo hiyo inamzuia mwanamke huyo kulainika
na kutokwa na vichocheo ambavyo vingemuwezesha afike kileleni kwa urahisi na
hivyo kumuona mumewe kuwa mwanaume wa ukweli.
Mbaya zaidi ni mwanamke ambaye mpenzi
wake anaonyesha kuwa anataka apate uhakika kuwa mpenzi wake wa kike amefika
kileleni. Mwanamke anapokuwa na mwanaume anaemtia presha ili afike kileleni na
yeye anajikuta hisia zake zinabadilika na kuwa tendo la ndoa kama kero fulani.
Hapo mwanamke huyo ataanza kudanganya
kuwa amfika mahali ambapo hajafika. Utaweza kuona uzito wa kero hiyo katika
mesiji iliotoka kwa dada mmoja isemayo hivi :
“Dr. Mimi napendwa na wanaume wawili na
tatizo nililokumbana nalo ni kwamba yule nisiempenda ndie ambae ananipa raha
kubwa ninapocheza nae ngoma ya wakubwa lakini huyu ninaempenda japo ana fedha
nyingi anaponihitaji kimapenzi naona kama usumbufu. Dr. nifanyeje nibadilishe
hali hiyo?”
Meseji hii inathibitisha kabisa utafiti
wa Dr. DAVID Barlow niliemtaja hapo juu kuwa mwanamke ambaye tayari ameshakuwa
na mpenzi kabla yako anapokulinganisha na mwanaume aliekutangulia anakosa amani
lakini hatakuambia hilo na kujikuta anakuwa na huzuni mara kwa mara.Mbaya
zaidi hali hiyo ikiendelea inaleta hasira kama dada mmoja
alivyonisimulia..
“DR.NIKO
kwenye ndoa mwaka wan ne mume wangu ananipa kila kitu ninachohitaji bila kujali
bei yake lakini kwenye tendo la ndoa ni mvivu na mara nyingine
ananikewepa.NILIKUWA NAMPENDA SANA lakini kutokana na hali hiyo katika
eneo la ngoma ya wakubwa nimejikuta nimeanza kumchukia.DR. UTANISAIDIAJE NIBADILISHE
hali hiyo? “
Tatizo la wanawake
kukosa hamu ya tendo la ndoa ni kubwa sana na linachangia kuharibu furaha
katika mahusiano mengi ya kimahaba. Tafiti ya hivi karibuni inaonyesha kuwa
moja ya tatu ya wanawake wenye umri kati ya miaka 18 – 59 wanakosa hamu
ya tendo la ndoa. Ni muhimu kutambua kuwa hamu ya tendo la ndoa ni
tofauti kabisa na uwezo wa mwanamke kujisikia raha ya tendo la ndoa
wakati linatendeka. Unaweza kuona kama jambo ambalo haliwezekani lakini tafsiri
zinathibitishwa kuwa wapo wanawake wengi ambao wanajishangaa kuona hawana hamu
ya tendo la ndoa lakini wanapojitoa muhanga na kufanya mchezo huo hupata raha
hadi kufika kileleni.
Kiongozi wa ufatifi
huo Profesa Alan Rilely wa chuo anasema kuwa ukweli huo wa kisayansi bado
unaonekaa sana miongoni mwa wanawake kati ya umri wa miaka 18 – 54 mwanamke
anapojitoa kumpa penzi mumewe ataweza kufika kileleni iwapo mumewe huyo anayo
maarifa ya kutosha katika kumwandaa mkewe kabla ya yeye kupanda jukwaani
na pia awe na uvumilivu wa kutosha kutumia muda mrefu katika kumwandaa
mkewe.
Mwanaume atumiapo
muda mrefu katika kumwandaa mwanamke anasababisha mwanamke atokwe na kichocheo
kingi cha OXIYTOCIN kichocheo ambacho hupunguza makali ya kichocheo kilelecho
hicho kiitwacho CORTISOL. Kupunguzwa kwa makali ya uchovu kunamruhusu mwanamke
aanzzw kupata raha japo mwanzoni alikuwa hana hamu ya kucheza ngoma ya wakubwa.
Katika hili ushahidi toka kwa mke wangu mwenyewe ambaye aliweza kufanya kukataa
kucheza ngoma ya wakubwa lakini nilipomchombeza akajikuta anafurahi na tukaweza
kucheza midundo mingi ya ngoma ya wakubwa. Kutokana na hali hiyo kujirudia mara
nyingi mke wangu siku moja aliniambia kuwa kusema maneno haya “usingekuwa
unapenda dini wewe ungekuwa muhuni sana”
Kwa wanawake wengi
ukosefu wa ukaribu wa kutosha na wapenzi wao husaidia wapoteze hamu ya tendo la
ndoa jambo ambalo wanaume wengi hawajui pale wanapojikuta wananyimwa nafasi ya
kucheza ngoma wanayoipenda sana. Ukosefu wa ukaribu unapunguza mshikamano wa
kihisia cemotional connection) na kumfanya mwanamke amwone mwanaume kama mzigo
badala ya kumuona kama sehemu yake mwenyewe utatambua kuwa mpenzi wako anakuwa
kama mzigo pale uonapo anakuwa mzito kukubaliana na wewe katika maeneo
mbalimbali ikiwamo kucheza ngoma ya wakubwa.
Wanaume wengine nao
huwa vimeo na kupata shida kukubali kuwa wamepoteza hamu ya tendo la ndoa na
hivyo kusababisha wake zao au wapenzi wao wa kike kuamini kuwa lazima watakuwa
na mchepuko. Mwanamke anapoona kuwa mumewe au mpenzi wake hana hamu na yeye na
kuamini kuwa ana mchepuko japo hana ushahidi wowote ni rahisi kwake kukubali
kuingia katika ulimwengu wa michepuko. Tatizo linakuwa kubwa zaidi pale
ambapo mwanamke ana hamu na mumewe na mumewe hana hamu na mke wake, katika hali
kama hiyo kwa kuwa mwanaume hataki aonekane kama kimeo (asieweza kazi ya kiume)
anakuwa mkali kwa mkewe. Hali hiyo imejirudia mara nyingi unakuta mwanaume
anakuwa mkali kwa mkewe katika makosa au madhaifu madogo madogo jambo
ambalo humuumiza sana mkewe. Maumivu hayo ya mwanamke yanamfanya awe mouongo
kufuatilia akili yake ya kimapenzi na hivyo kutengeneza hali ya mchepuko.
Katika mazingira kama
hayo hata pale mwanaume atakapokuwa na hamu na mkewe na mkewe atakuwa katika
hali ya ukavu kutokana na uvhungu uliosababishwa na ukali wake yeye mwenyewe.
Mwanamke huyo anapojikuta anakuwa mkavu kwa mumewe jambo ambalo halikuwepo
kabisa anashindwa kukubali kuwa sasa tayari amekuwa kilema katika eneo hilo na
hivyo kujaribu kucheza na mwanaume tofauti. Kilichonisababisha kuandika mada
hii ni kutokana na simu mbili toka wanawake wawili tofauti ambao wamejikuta sio
vilema baada ya kuchepuka nje ya ndoa zao. Kujiona kuwa sio wa kutamanika,
kujivunia maumbile ya mwili wako ni jambo la muhimu sana katika kusababisha
vichocheo vya hamu ya ngoma ya wakubwa kufanya kazi vizuri.
Ukiwa mnene, matiti
madogo au bunduki ya kiume ndogo, makalio madogo au mfupi wa kimo, ukiwa
mweusi na unatamani ungekuwa mweupe hayo yanapoingia akilini mirija ya
vichocheo inasinyaa kushindwa kuleta mtiririko mzuri wa hamu ya
ngoma ya wakubwa. Pale mtu anapojiona kuwa hana maumbile ya kutamanika
anajikuta hafikirii sana juu ya raha ya tendo la ndoa, mtu anapokuwa hafikirii
mara kwa mara juu ya tendo la ndoa anashindwa kutengeneza kiwango
cha kutosha cha kichocheo cha TESTOSTERONE ambacho husababisha hamu ya tendo la
ndoa miongoni mwa wake kwa waume.
Utafiti wa miaka 33
unaonyesha kuwa asilimia 15 ya wanawake wanaotumia vodonge vya majira kuzuia
kupata ujauzito wanapoteza hamu ya kucheza ngoma ya wakubwa. Kiongozi wa
utafiti huo daktari bingwa wa mambo ya wanawake (GYNECOLOGIST) Dr. Lee sharman
anasema wanawake wengi wanasingizia idonge hivyo jambo ambalo sio la kweli.
Utafiti huo uliohisisha wanawake 8,400 ulionyesha kuwa asilimia 22 hamu ya
tendo la ndoa iliongezeka, asilimia 63 hawakuona badiliko lolote lile na
ni asilimia hiyo 15 tu ndio walioona upungufu wa hamu ya tendo la ndoa.
Dr. Lee anasema
wanawake hao huona hicho kuwa kisingizio rahisi kwa kuwa hawataki
kuangalia maeneo mengine yenye uwezo mkubwa wa kuwapunguzia hamu ya tendo la
ndoa kama woga wa kuhoji mambo, kuogopa migogoro, ukosafu wa uwazi,
kushindwa kumweleza mwanaume kuwa ameshindwa kazi ya kiume au ana maumbile
madogo na kadhalika.
Uhusiano wa kimapenzi
unahusu mambo mengi kama maongezi, fedha, usafi, zawadi kukosoana na sio tendo
la ndoa peke yake lakini ukiondoa tendo la ndoa mengine yote yanakosa
nguvu za kushiriki uhusiano wa kimapenzi. Tatizo ni kwamba watu wengi
hawajui kuwa tendo la ndoa linaweza kuongezea nguvu mambo mengine na
hivyo kufanya bidii kubwa katika hilo. Tatizo ni kwamba ukifanya bidii katika
eneo hilo na ukapuuzia maeneo mengine utakuwa unatengeneza upinzani wa
wewe kufurahia tendo la ndoa toka kwa mwenzio japokuwa anakupenda.
Na sio hilo tu bali pia ukifanya bidii katika maeneo mengine na kupuuzia tendo
la ndoa lazima utazua mgogoro kati yenu.
Watu wengi
wanashindwa kuwa makini katika maeneo mengi ya kimahusiano lakini ni wepesi
sana kulaumu pale mpenzi anapomwacha au kumsaliti. Ni kweli kabisa kuwa mwisho
wa uhusiano unaumiza sana bila kujali nani amesababisha hilo lakini wengi
hawachukui tahadhali. Unaweza kusema kuwa hata ungefanya nini kama mtu
atakuacha atakuacha tu, hivyo ni kweli lakini pale unapoachwa
JE NGOMA YA WAKUBWA
YAWEZA KUVUNJA NYUMBA?
Tunaposikia watu
maarufu hasa wasanii wamevunja mahusiano yao huwa tunashangaa sana kwa kuwa hao
ni watu wenye fedha nyingi sana na kutokana na umaarufu wao usingetegemea hali
hiyo kutokea. Mara nyingi tunasikia kuwa usaliti, ulevi au fedha ndio vitu
vinanvyochangia ndoa nyingi kuvunjika lakini hatusikii kuwa matatizo ya nguvu
za kiume, ukubwa wa maumbile au udogo wake au ukosefu wa ufundi wa kutosha
katika uchezaji wa ngoma ya wakubwa kuwa ni visababisho ukweli ni kwamba
madhaifu katika eneo la tendo la ndoa yamewaleta wengi sana katika ofisi yangu.
Mwanzoni mwa uhusiano
mara nyingi kila mmoja anajiona kuwa ni mwelewa na yanakuwepo matarajio kuwa
huenda madhaifu hayo yatatokomea baada ya muda Fulani jambo ambalo kwa wengi
halitokei. Pale inapokuwa wazi kuwa tatizo halitatokomea, huzuni na hali
ya kukweka kushiriki kucheza ngoma ya wakubwa wanatokea. Hali hii humfanya
mmoja au wote wawili kujisikia upweke ndani ya nafsi yake na upweke huo
hubadilika kuwa uchungu na mwishowe kuwa hasira. Inapotokea kuwa ni mmoja
ambaye ana tatizo, fedheha na kujiona kama kimeo itasababisha awe mkimya au
atumie ukatili kumkwepa mpenzi wake anayependa wacheze ngoma ya wakubwa mpenzi
ambaye hana tatizo atajisikia vibaya kuomba apewe kitu ambacho mpenzi wake
hapendi kukitoa.
Hali hiyo
isipotafutiwa ufumbuzi yule asie na tatizo ataanza kuwa mtu mwenye hasira
katika maeneneo mengine tofauti na ngoma ya wakubwa. Hatari ni kwamba tatizo
hilo linapokuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu linasababisha mmoja kujitenga
kihisia na kuonekana hana uchangamfu uliokuwepo mwanzoni. Mpenzi anapojitenga kihisia
kutokana na kero ya kunyimwa anachokipenda na mtu anayedai kuwa anampenda
inakuwa vigumu sana kurudia hali ya uchangamfu ule wa mwanzoni.
Tafiti zinaonyesha
kuwa asilimia 43 ya ndoa zinazovunjika mzizi wake ni udhaifu au ujinga katika
kucheza ngoma ya wakubwa na watafiti hao wanasema kuwa idadi inaweza kuwa kubwa
zaidi ya hiyo kutokana na wengi kukwepa kukubali kuwa wameshindwa kucheza
vizuri. Kiongozi wa utafiti huo Dr. Sari Eckler Cooper anasema kuwa pale uonapo
ndoa inavunjika kutokana na usaliti ni kwamba yule aliechoka kutokana na
kunyimwa mchezo au kutoridhika na utamu wa ngoma ya wakubwa anaamua kusaliti
ili asababishe kuachana na yule anaemuona kuwa kimeo katika kucehza
ngoma ya wakubwa. Watu wengi wanadai kuwa jambo kubwa linalosaidia kudumisha
ndoa ni uvumilivu na mimi napingana na jambo hilo japo naamini kuwa uvumilivu
ni jambo zuri. Unapovumilia jambo lazima liwepo tumaini kuwa hali hiyo
itabadilika kwa kuona bidii ambayo mwenzio anaifanya kuleta mabadiliko.
Iwapo mpenzi wako alien a udhaifu Fulani anafahamu jinsi udhaifu wake
unavyokukosesha raha na asifanye bidii ya kuleta mabadiliko huo ni
ukatili mkubwa usiohitaji uvumilivu kabisa kutokana na imani yangu hiyo kuwa
lazima uvumilivu uwe na mpaka nilijikuta siku moja nasema kitu ambacho hata
mimi mwenyewe kilinishangaza.
Dada mmoja katika
ofisi moja alisema “Ndoa ni kuvumiliana” na mimi haraka sana nikasema
“Kuvumiliana kumewekewa mbwa, mbwa wanapofanya mapenzi wanafuatana na hata
ukipiga mbwa jike na mbwa dume haachani wanavutana pamoja na kubakia wemenatana
hivyo”. Baada ya kutamka jambo hilo ambalo lilikuja bila kupanga nilijikuta
nimeanza kufikiria juu ya ukweli wa lile nililosema. Mbwa wanajikuta katika
hali hiyo lakini hali hiyo haidumu siku nzima kwani baada ya muda fulani huachiana
jambo ambalo linatupa picha ya kwamba unapovumilia jambo lazima liwepo tumaini
ya hali kubadilika na kuwa kama ile ya mwanzoni kinyume na hivyo ni gereza la
mateso.
Upo uwezekano mubwa
wa mwanamke kupungukiwa na hamu ya tendo la ndoa baada ya kujifungua jambo
ambalo linatoa mwanga kwanini raha ya ndoa hupungua katika miaka 2 – hadi 5 ya
mwanzoni. Kutokana na uchovu wa kipingi cha ujauzito, wasiwasi wa siku ya
kujifungua inapokaribia, ukosefu wa usingizi baada ya kujifungua na kubadilika
kwa maumbile ya uzazi baada ya kujifungua vinamuathiri sana mwanamke. Mama
anaponyesha mtoto upo uwezekana wa kichocheo kiitwacho ESTROGEN kupungua na
hivyo kusababisha viungo vya uzazi kuwa na ukavu ambao mwanzoni haukuwepo.
Wanawake wanashauriwa kutumia mafuta ya K.Y Jelly kuondoa ukavu huo.
Kipindi hiki ni
kipindi kigumu sana kwa wanaume wasioelewa hali halisi baada ya mwanamke
kujifungua. Inashauriwa mwanamke aanze kushiriki ngoma ya wakubwa baada ya wiki
sita toka siku aliyojifungua na wanaume wanapashwa kuheshimu hili kuepuka
ugomvi au chuki baina yao. Pamoja na hilo ni muhimu kukumbuka kuwa baada ya
kujifungua mwanamke hatakuwa na hamu kiasi kile alichokuwa nacho mwanzoni na
kwa baadhi ya wanawake inaweza kuchukua mwaka mzima kuweza kurudia kasi ya
mwanzoni. Halii hiyo inasababishwa na kichocheo cha PROLACTION ambcho hutoka
kwa wingi kwa mama anayenyinyesha. PROLACTIN hupunguza hamu ya mwanamke kucheza
ngoma ya wakubwa kwa kupunguza mtiririko wa kichocheo cha hamu kiitwacho
ESTROGEN.
Hapa ningependa kutoa
angalizo ambalo wengi wanhitaji kulisikia. Mwanamke anapokaribia kujifungua
mishipa ya damu iitwayo VEIN katika viungo vya uzazi hupanuka kuliko kawaida
yake na hivyo kufanya kuta zake kuwa dhaifu sana. Kuna hatari ya kifo iwapo
mwanaume kwa kutumia mdomo wake atachezea maeneo ya viungo vya uzazi vya
mwanamke miezi miwili kabla ya kujifungua au miezi miwili kabla ya
kujifungua. Mwanaume akitumia mdomo wake bila kujua anaweza kusababisha
hewa kuingia kwenye mishipa hiyo ya vein na kusababisha damu kutofika kwenye
ubongo wa mwanamke na kusababisha kifo. Hali hiyo iitwayo AIR EMBOLISM mara
nyingi hutokea iwapo mwanamke atashiriki ngoma ya wakubwa kabla ya wiki 6
kuisha.
Jambo linguine la
ajabu linalojitokeza pale mama anapojifungua ni kwamba ile hali ya kunyonyesha
mtoto mama anapoteza hamu ya kuguswa na mumewe kwa kuwa tayari anakuwa amepata
mguso wa ngozi kwa ngozi toka kwa mtoto na kuona kuguswa na mumewe kama kero ya
aina fulani. Wapo wanawake wengine ambao hujisikia raha ya kimahaba pale mtoto
anayonyonya chuchu PENZI LINAPOGEKA KUWA KERO
Mahusiano ya kimapenzi ni kitu kizuri
sana ndio maana mara ya kwanza mtu anapoingia katika mahusiano ya kimapenzi
anakuwa na furaha kubwa sana. Naomba uzingatie kuwa nimesema kuwa mtu
anapoingia katika uhusiano kwa mara ya kwanza, yaani kama ni
mwanaume huyo anakuwa ndie mwanamke wa kwanza kabisa kwake
na kwa mwanamke huyo ndio anakuwa mwanaume
wa kwanza kabisa. Katika ulimwengu tulionao sasa ni mara chache sana
utaona kuwa mwanaume ambaye hajawahi kuwa na mahusiano ya kimahaba NA
MWANAMKE anaanza na mwanamke ambaye na yeye huyo ndio anaekuwa mwanaume wa
kwanza.
Tatizo tulilonalo sasa utakuta mwanaume
ambaye tayari ameshakuwa na mahusiano na wanawake 2 anaanza uhusiano na dada
ambaye hajakuwa na uhusiano wowote au dada ambaye ameshakuwa na mahusiano na
wanaume wawili anaanza mahusiano na mwanaume ambae hajawa katika mahusiano ya
kimapenzi.Katika mazingira kama hayo lazima mtu atajikuta analinganisha mpenzi
aliene sasa na Yule aliemtangulia.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )