Muandishi : Eddazaria g.Msulwa
Ilipoishia
Askari
mmoja mwenye mwili mkubwa akamnyanyua Fetty na kumuweka begani mwake na
safari ikaendelea.Fetty akayafumbua macho yake na kuona askari aliye
mbebe ndio wa mwisho katika mstari wanao tembea,Kwa ustani wa hali ya
juu Fetty akaichomeka mikono yeke katikati ya shingo ya
askati,kwakutumia pigu akaanza kumnyonga askari huku akiwa amening'inia
kwa nyuma.Mikoromo ya asakri ikawastua wenzake waliopo mbele kitendo cha
wao kugeuka wakamkuta mwenzo ndio yupo kwenye hatua za mwisho huku
macho yake akiwa ameyatoa njee
ENDELEA
Askari
mmoja akataka kufyatua risasi ila mkuu wa masafara akamzuia,Fetty
akaiachia shingo ya askari huku akiwa amehakikisha kwamba askari huyo
yupo kwenye hali mbaya sana.Askari mmoja akampiga Fetty kwa kutumia
kitako cha bunduki na kumfanya Fetty ajikunje huku akitoa mguno mkali
wa maumivu
“Kumbukeni kuwa,anahitajika akiwa hai”
Mkuu wao alizungumza
“Sawa mkuu,ila anahitaji kupata kibano kidogo”
Wakaendelea
kumtazama mwenzo,ambaye hadi hapa alipo hali yake haipo vizuri
sana.Vichwa vya askar vikaanza kupata moto kwani mwenzao ambaye alikuwa
anakaribia kunyongwa ndio anaye fahamu njia ya bombo hilo japo imenyooka
ila kuna sehemu mbele imegawanyika katika njia nne.Mwenzao
anayejulikana kama inspector Julio hawezi kuendelea mbele na safari
“Mkuu kuna tatizo jengine limejitokea,Over”
“Nini tena inspector John? Over”
“Huyu binti alimkaba Inspector Julio,Over”
“Nyinyi mulikuwa wa hadi mwenzetu akabwe?”
Sauti ya mkuu wao ilizungumza huku akiwa anafoka,
“Mkuu alizimia,ndipo inspector Julio alipo amua kumbeba”
“Pumbavu zenu.Hakikisheni anatoka huyo binti,akiwa hai na Julio naye akiwa hai”
Fetty
akatabasamu huku akiwatazama askari,kwani kwake kazi yake imeshaanza
kuwa nyepesi kwani mtu ambaye anamuhofia ni huyu Inspector Julio,ambaye
kwa mtazamo wake tu anaonekana ni mtu hatari sana katika swala zima la
kutumia silaha.Askari mmoja akasimama mbele ya Fetty huku akiwa amempa
mgongo akisaidiana na wezake katika kumpa huduma Inspector Julio,huku
kazi yake ikiwa ni kuzifungua kamba za viatu vya Julio
Kwa
umakini wa hali ya juu,Fetty akazichomoa funguo nyingi zinazo ning’inia
kiunoni mwa askari huyo pasipo yeye mwenyewe kujua.Kwa bahati nzuri
katika wingi wa funguo hizo zipatazo kumi na mbili,mbili ni funguo za
pingu.
Macho
ya Fetty yakawa na kazi ya kuwatazama askari jinsi wanavyo pata shida
katika kumsaidi mwenzao ambaye hali yake inazidi kuwa mbaya.
Hakuna
askari aliye kuwa na muda wa kumtazama Fetty kwani wanaamini kile
kitako cha bunduki alicho pigwa kwenye tumbo,bado anaendelea
kukisikilizia maumivu yake.Fetty akafanikiwa kufungua pingu za mikono
pasipo askari yoyote kugundua.Akajaribisha kufungu mnyororo wa miguni
ila akashindwa kwani hakuna funguo inayo ingiliana na kufuli alilo
fungwa miguuni.
“Ja............ama..ani
mmmim...i siwezi ku...pona.Ila,njia uki...oony......sha utaku...nja
kulia...kwenye shimo lenye mlang....o wa....”
Inspector Julio alizungumza kwa shida na hakuweza kumalizia sentesi yake,mauti yakamchukua.
Inspector
John akanyanyuka kwa hasira na kumfwata Fetty sehemu aliyo kaa.Kufumba
na kufumbua akajikuta akirushwa juu kimo cha mbuzi tena beberu na kutua
chini kama mzigo.
Hii
ni baada ya Fetty kuikutanisha miguu yake kwa pamoja,Kisha mikono yake
aliikita chini na kujizungusha kwa kasi kubwa.Askari walio salia wakiwa
wanamtizama mkuu wao.Fetty akajinyanyua kwa haraka na kumvaa askari
aliye mchomolea funguo,akaichomoa bastola ya askari huyo ambaye
alijitahii kumpiga ngumi za mbavu Fetty
Bila
ya huruma Fetty akafyatua risasi iliyo penya kwenye kichwa cha akari
anayepambana naye na kumtuliza kimya.Askari watatu wa kiume wakazikoki
kwa haraka bunduki zao na kuanza kuzifyatua risasi,ila kwa haraka sana
kama tairi la gari liendalo kwa kasi sana,akawa na kazi ya kubiringika
huku akiwafwata askari kwenye miguu yao mita chache kutoka alipo.
Akiwa
anabiringika, bastola iliyopo mkononi mwake ikawa na kazi ya kufyatua
risasi zilizo waangusha askari watatu chini na akabaki Inspector John na
askari wa kike aliyetengenezwa kama yeye,na wakati wote tukio la
wezake kuangamizwa lilimpa kiwewe hadi akawa na kazi ya kuyaziba masikio
yake akiziba asisikie milio ya risasi.Fetty akalala katikati ya miguu
ya Inspector John huku mdomo bastola yake akiwa ameuweka kwenye sehemu
za siri za Inspector John.Bunduki ya inspector John akawa ameilekezea
kwenye kichwa cha Fetty ambaye macho yake yanatazamana na macho ya
Inspector John
“Shoot ni kushooti”
Fetty alizungumza huku akitabasama,na bastola yake akawa na kazi ya kuigusisha gusisha kwenye vitenesi vya Inspector John
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )