Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli amevunja
Baraza la Madiwani rasmi baada ya serikali kuigawa manispaa hiyo kuwa
mbili. Kagurumjuli alilivunja juzi saa 11:00 baada ya kumalizika kwa
Baraza la Madiwani la kawaida.
Alipokuwa
akitangaza kulivunja baraza hilo, Kagurumjuli alisema amevunja baraza
hilo kwa kuwa serikali imegawanya manispaa hiyo kuwa wilaya mbili, ya
Kinondoni na Ubungo hivyo kwa kuwa wilaya zote tayari zina wakurugenzi,
wakuu wa wilaya na makatibu tawala wa wilaya imempasa kufanya hivyo.
“Baraza la madiwani limevunjwa, kuvunjwa kwa baraza hili ni ukomo wa meya pia,” alisema.
Aliongeza kuwa wiki ijayo kutakuwa na uchaguzi wa meya katika manispaa hizo.
Meya
wa Manispaa ya Kinondoni alikuwepo kabla ya kuvunjwa kwa baraza hilo ni
Boniface Yakob ambaye amebaki nafasi yake ya udiwani.
Kuvunjwa kwa baraza hilo kulikuwa kunatarajiwa baada ya serikali kugawanya manispaa ya Kinondoni kuwa mbili.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )