Featured
Loading...

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 29 & 30

MWANDISHI : EDDAZARIA

ILIPOISHIA
Mtu huyo wa ajaba akaendelelea kutazama tazama kila kona ya sable hii, akapiha hatua mbili mbele na kuzama ndani kabisa ya sable hii, na kuwapa mgongo Rahab na Raisi Praygod walio simama nyuma yake. Akaendelea kuvuta vuta pumzi, iliyo muashiria kwamba humu ndani kuna binadamu waklio hai, akalikoki bunduli lake aina ya gobore na kulishika vizuri huku kidole chake kimoja akiwa amekizamisha kwenye traiga, kwa haraka  akageuka nyuma na kuwaona Rahab na Raisi Praygod wakiwa nyuma yake wanamtazama

ENDELEA
Kwa haraka Rahab akaruka hewani na kuipiga teke bunduki ya mtu huyu mwenye muonekano wa ajabu sana, bunduki yake ikaanguka chini na kumpa nafasi nzuri Raisi Praygod kumrukia mtu huyo kwa kutumia bega lake lililo tua begani kwa mtu huyo na wote wawili wakaanguka chini.

 Rahab kwa haraka akaiokota bunduki ya mtu huto na kwakutymia kitako cha bunduki hiyo aina ya gobore akampiga nayo kichwani zaidi ya mara kumi mtu huyo, na kupelekea kichwa cha mtu huyo kupasuka kwa na kuvuja damu yenye rangi nyeusi ti.
“Mtu gani huyu….?”
Rahabu aliuliza huku akihema kwa nguvu akionekana kuchanganyikiwa kwa kumuona mtu wa aina hii ambaye tangu azaliwe hajawahi kumuona.

“Tuondike hakuna haja ya kuendelea kukaa hapa”
Raisi Pragod alizungumza huku akichungulia mlangoni kutazama kama wale watu wengine wa kutisha wamesha ingia ndani walipo kua wakiingiza mizoga ya watu walio waua. Wakatoka nje wakiwa katika tahadhari kubwa huku Rahab aklwa ameishika bunduki ya mtu huyo.

Wakafanikiwa kutoka nje pasipo kuonekana na watu hao ambao wapo ndani ya kijumba chao wakiendelea kuwakata kata vipande marehemu walio wachukua na kuwafanya ndio chakula chao cha usiku. Wakaanza kutokomea porini huku wakimuomba Mungu waweze kutoka kwenye msitu huu ambao bado haujawapa matumaini ya kuweza kuziokoa nafsi zao zilizo kwenye matatizo makubwa

Hasili ya watu hawa wa kutisha wanajulikana kama Mazombi, walio anza kujitokeza mwaka 1819 katika bara la ulaya. Inasemekana watu hawa ni wale walio weza kupoteza maisha kwa sumu zenye kemikali kubwa na waliweza kurudi katika ulimwengu huu wakiwa katika hali hiyo ya kutisha na kuweza kuwafanya wanadamu halisi kama ndio vitoweo vyao vya kila siku.

Rahab na Raisi Praygod wakaendelea kukata mbuga pasipo kuchoka, japo wanatamani kuweza kupata japo dakika waweze kupumzika, ila kila walipo kumbuka maiti za watu walio waona wakishushwa na mazombi hayo hawakutamani kamwe kuweza kusimama.

Hali ya majonzi ikawatawala mazombi walio mshuhudia mwenzoa aliye pasuliwa kichwa na kusababisha ubongo wote kumwagika nje. Hawakua na hamu hata ya kuendelea kupata vitoweo walivyo kuja navyo na ziadi kila mmoja akachukua silaha yake na kuingia msituni kufwatilia watu hao walio sababisha mauaji ya mmoja wao. Kutokana na kuufahamu vizuri msitu wao, wakajigawa kwenye makundi ya mazombi wawili wawili na kupelekea kuwa na vikundi vinne. Kila mmoaja akajiapiza kuweza kufanya mauaji ya kikatili kwa watu walio sababisha mauji ya mpendwa wao
                                                                                                    ***
Samson na wezake wakafanikiwa kufika katika kiswa cha Kunashir nchini Russia, kwa bahati nzuri wakafanikiwa kupokelewa na mkuu wa kikiso kilicho asi nchi ya Russia bwana Rusev, Wakapelekwa moja moja kwa moja kwenye jengo lenye ofisi za kikundi hichi kinacho endelea kufanya mapinduzi kwenye nchi yake ikiitaka serikali kuweza kuunda serikali mbili, ili wao  wajipatie mamlaka ya kuweza kutengeneza silaha hatari za nyuklia.

Kila mmoja akakabidhiwa kinywaji alicho kihitaji yeye, ili kuweza kujipozwa kwa uchovu mwingi wa safari yao ndani ya maji, tangu pale walipo kamtwa na jeshi la polisi nchini Tanzania. Fetty na wezake hawakuwa na uwezo wa kuielewa lugha ya kirusi, ambayo Samson yeye aliweza kuizungumza vizuri pasipo matatizo ya aina yoyote. Alicho kua akikifanya Samson ni kuwatafsiria kila kitu ambacho alicho kua akikizungumza na bwana Rusev.

“Jamaa anauliza eti, tunaweza kujiunga na kundi lake?”
“Mmmm……!!” Anna aliguna
“Hatuwezi sisi tupo hapa kwa ajili ya biashara”
Samson akamjibu bwana Rusev kitu alicho kizungumza Fetty anaye onekana kuto kubaliana na swala zima la wao kujiunga na kundi la bwana Rusev
“Je anauliza tunahitaji kiasi gani cha pesa ili tuweze kumkabidhi hii manohari?”
“Sasa hapo ndio umenena la maana” Halima alizungumza huku akitabasamu
“Anatulipa kwa dola au shilingi?” Agnes aliulza
“Hembu na wewe acha ushamba wako, huku shilingi aitolee wapi?” Fetty alimkosoa mwenzake
“Haya yaishe kiongozi Fetty”
“Muambia sisi tunataka dola milioni mia zinatutosha”
Samson akamgeukia bwana Rusev na kumueleza kiasi walicho kitaja wezake na bwana Rusev hakuwa na hiyana zaidi ya kukubali kuwalipa kiasi hicho.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top