Ina ladha ya uchachu mkali na utamu wa mbali kwa wakati mmoja.
Hufungwa katika majani ya migomba ili kuhifadhi ubichi wake. Kawaida
huvunwa asubuhi sana na kuuzwa mchana wake au usiku wake, kila inavyokaa
sana hupunguza ubora wake kwa walaji na thamani yake.
Na kwa sababu
walaji wa Tanzania hutegemea zaidi Mirungi kutoka Kenya, huwa hawapati
ule ubora unaopakikana kutokana na umbali na kutofika kwa haraka; ingawa
walaji wa Arusha hupata haraka zaidi kwa ukaribu wake na Nairobi kuliko
wale wa Dar na Zanzibar au miji ya bara ya mbali kama Mwanza na
kwengineko.
Mirungi (Khat) au (Catha edulis) Ni mmea au mti unaoota au kuoteshwa.
Mirungi ni mti unaoota polepole ambao unakuwa kwa urefu wa mita 1.5
hadi mita 20, kutegemea na eneo kijiografia na pia hali ya mvua ya eneo.
Likiwa na majani ya kijani yaliyokoza ambayo yana urefu wa sentimeta 5
hadi 10 na upana wa sentimeta 1 hadi 4.
Kemia ya Mirungi (khat)
Muundo wa Cathinone
Mirungi (khat) inakusanya ndani yake alkaloid mbili ambazo ni Cathine
na Cathinone. Alkaloid hizi zinafanana sana na familia ya kundi la
kemikali linaloitwa PPA ( phenylpropanolamine) ambalo ni kundi dogo la
phenethylamines linalofanana na kundi la kemikali la catecholamine na
amphetamine kama kichangamsho (stimulant) ambayo inasemekana husababisha
msisimko, uchangamfu, kuwa na aina ya furaha ya kuwazika –kuhandasika-
na huondosha hamu ya kula na kusababisha ukosefu wa usingizi.
Tuachane na haya ya kikemia. Uvunaji wa mirungi huhitaji umakini wa
hali ya juu kwani kemikali mojawapo ambayo ni cathinone hupotea hewani
kirahisi kama kama mmea huu utaachwa ukauke ndani ya masaa 48, hivyo
bhasi wavunaji huhifadhi mirungi kwenye mifuko ya plastiki na
kuizungushia majani ya migomba kipindi wanasafirisha ili kuifanya
isipoteze kemikali muhimu ya cathinone. Wakati mwingine huzihifadhi
ndani ya maji ili zisipoteze ubora wake.
Mnamo mwaka 1980 WHO (Shirika la Afya Duniani) liliiweka Mirungi
katika fungu la madawa ya kulevya ambayo inasababisha nafsi kutawaliwa
nayo au kuwa na uraibu (addiction) kwa daraja ya kati hadi ile yenye
nguvu. Watumiaji wake hujitetea kwa kuamini kuwa majani hayo huwapatia
nguvu, na uchangamfu na mliwazo wa furaha.
Madhara ya muda mfupi yatokanayo na matumizi ya mirungi (khat)
• Kujiamini kupita kiasi
• Magonjwa ya vidonda vya tumbo (ulcers)
• Shikizo la damu
• Ukosefu wa hamu ya kula chakula (loss of appetite)
• Upungufu wa hayaa na Kukosa usingizi (insomnia)
• Kuongezeka kwa mapigo ya moyo
• Kukosa haja kubwa (constipation)
• Uropokaji, uchache wa adabu, ujuaji wa kila kitu
• Kukosa usikivu na utulivu
• Magonjwa ya akili
• Tahadhari

Madhara ya muda mrefu
• Huzuni/mfadhaiko wa mawazo
• Upungufu wa msukumo wa kufanya jimaa (sex drive). Na pia kuwahi kumaliza haraka na kutoweza kudumu kwenye tendo la ndoa kwa muda mrefu (pre-ejakulation)
• Humpelekea mlaji kutawaliwa nayo (Addiction)
• Msongo wa mawazo
• Kupata njozi zinazojirudia rudia
• Mahangaiko ya akili
• Kushindwa kujizuia kufanya vitendo visivyofaa kwenye jamii.
• Kuwa kwenye hatari kubwa ya kupata Shambulio la moyo
• Utumiaji wa muda mrefu husababisha kuharibu utendaji kazi wa ini, na pia kusababisha ubadilikaji rangi meno, kudhoofika, na fizi kuuma na harufu ya mdomo
• Kansa ya mdomo

Athari zisizozuilika
• Kifo
• Kiharusi kutokana na shambulio la moyo
• Kifo
• Kiharusi kutokana na shambulio la moyo
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )